nani_said.fw

Dr. Said Said ni daktari, mfanyabiashara, mwanablogu na dereva Mkuu wa kampuni ya Online Profits.

Japokuwa yeye ni daktari (MD) kitaaluma, uzeofu wake wa mambo ya mauzo na masoko (hususan katika mtandao) umetokana na kushiriki katika biashara tofauti za kwenye mtandao (online) na zisizo kwenye mtandao (offline) kwa zaidi ya miaka 12.

Hivi sasa uzoefu mkubwa wa Dr. Said upo katika;

  1. Mauzo ya ana kwa ana (One on One sales)
  2. Masoko Ya Mtandao (Online Marketing) hususan mtandao wa Facebook na
  3. Kutengeneza Mashine ya mtandao yenye uwezo wa kunasa wateja wanaohitaji bidhaa na huduma unazotoa.  😉 (Developing online marketing/sales funnels)

Historia Ya Dr. Said Said

Elimu:

2004 – 2009: Doctor Of Medicine (MD) kutoka Chuo Cha KCMC

2003 – 2006: Safari Ya Mafunzo Ya Utengenezaji Wa Tovuti Na Mauzo Ya Ana Kwa Ana

Alikuwa ni mtu wa mauzo wa kujitegemea (independant sales representative) katija jiji la Dar Es Salaam na Tanzania kwa ujumla kwenye kampuni yenye kuuza bidhaa zenye kuwafunza watu kompyuta.

Kampuni hii ilikuwa inaitwa BizNas na makao yake makuu yalikuwa mji wa Dubai.

Japokuwa Dr. Said hakusoma chuo cha kompyuta, bidhaa zilizokuwa zikitolewa na kampuni hii zilimpa Dr. Said elimu ya msingi ya kompyuta na kumfunua macho kuhusu utengenezaje wa tovuti.

Vile vile uwezo wa kuuza bidhaa ana kwa ana (One on One sales) amejifunzia hapa baada ya kuhangaika sana mitaani kujaribu kuuza hizo bidhaa.

2007 – 2013: Safari Ya Mafunzo Ya Uongozi

Baada ya kampuni ya BizNas kupata matatizo, Dr. Said alijishirikisha na kampuni ya QNet, kampuni yenye kuuza bidhaa za afya (wellness), mawasiliano (telecommunication), mapumziko (Resorts) na bidhaa za mapambo (jewellery).

Ujuzi wa kutengeneza tovuti aliopata Dr. Said kwenye kampuni ya BizNas pamoja na kampuni ya QNet, ulimwezesha kufanya mauzo ndani ya Tanzania na nchi za nje ikiwemo Malaysia, UK, Papua New Guinea, DRC n.k kupitia mauzo ya ana kwa ana na tovuti yake binafsi.

Vile vile Dr. Said alikuwa mmoja katika viongozi wa mauzi na kuwaongoza watu si chini ya 500 katika elimu ya masuala ya masoko na mauzo.

2012 – 2014: Safari Ya Mafunzo Ya Utengenezaji Wa Tovuti Za Kisasa

Aliamua kusimama mwenyewe kwa kuanzisha kampuni yake Strategic Marketing & Design yenye kurusha na kutengenezea tovuti za kisasa kwa wafanyabiashara wa Arusha na Tanzania kwa jumla na vile vile kuwasaidia wafanyabiashara kupata masoko kupitia mtandao.

Zaidi ya tovuti 30 zilitengenezwa kwa muda huo na Dr. Said alishiriki katika utengenezaji wa zaidi ya asilimia 80 tovuti hizo.

Na ndio hapa Dr. Said amepata kuelewa kiundani jinsi gani ya kutengeneza tovuti za kisasa zenye kunasa watu wenye kuhitaji bidhaa au huduma unazotoa.

2013 – 2014: Safari Ya Mafunzo Ya Utengenezaji Wa Tovuti Zenye Kunasa Wateja Kama Smaku 😉

Japokuwa Dr. Said alikuwa anaendesha kampuni yake ya Strategic Marketing & Design, alikuwa na kiu kubwa ya kuelewa kiundani jinsi wanasoko wa mtandao  (online marketers) wanaweza kutumia tovuti yao kuwauzia bidhaa wateja husika bila ya kuonana nao wala kuongea nao. Mchakato wote wa mauzo ulikuwa ukifanywa na tovuti.

Alijiunga katika kampuni ya Empower Network kwa lengo la kujifunza na kuwa mwana mauzo wa mtandao (affiliate marketer).

Alijifunza sana mambo ya mauzo kupitia mtandao (Online Marketing) na akaweza kuwafundisha watanzania wengine waliokuwa hawana uzoefu na wao kuweza kufanya mauzo.

Ndipo hapa Dr. Said alipojifunza jinsi ya kutengeneza mashine ya mtandao yenye kunasa wateja husika na kuwafanyia mauzo.

January 2016 Mpaka Sasa: Safari Ya Kukusaidia Wewe Kupata Wateja Wenye Hamu Ya Bidhaa Na Huduma Zako Kuptia Mtandao

Lengo la Dr. Said kuanzisha kampuni hii ya Online Profits ambayo ni uboresho wa kampuni ya Strategic Marketing & Design ni kwa ajili ya kuwaongoza wafanyabiashara kama wewe kupata elimu na nyenzo zitakazokupatia wateja mara kwa mara kwenye biashara yako kupitia mtandao.

ushauri bure kutokakwa Dr. Said

Makala Zilizochapishwa Na Dr. Said

Dr. Said ameandika na kuchapisha makala tofauti kwenye mada ya masoko (marketing), mauzo (sales), stratejia za biashara na maendeleo binafsi (personal development).

Makala zake zimechapishwa na magazeti na majarida tofauti ikiwemo Arusha Times, Daily news, The Guardian, The Citizen na Man Magazine.

Mafunzo Aliyohudhuria:

Dr. Said amehudhuria katika mafunzo tofauti ndani na nje ya nchi (kama Kenya, Malaysia na Singapore) akiwa kama mhudhuriaji na vile vile mkufunzi katika maada yenye kuhusiana na:

  1. Uongozi Katika Biashara
  2. Mauzo
  3. Masoko na
  4. Maendeleo Binafsi

Mapenzi (Hobbies) Ya Dr. Said:

Dr. Said ana mapenzi makubwa wa usomaji wa vitabu vyenye mada ya uongozi, ujasiriamali, mauzo/masoko na psycholojia ya mafanikio (success psychology) na amesoma zaidi ya vitabu 50 na mamia ya blogu katika mada hizo. Na vile vile Dr. Said amejisajili katika kozi tofauti zenye kuendeshwa na wanamasoko (wa mtandao) na wafanyabiashara wakubwa duninani.

Dr. Said anapenda sana mtandao wa intaneti. Anavutiwa sana na jinsi gani ujumbe mdogo unaweza kuwafikia mamilioni ya watu ndani ya masaa machache, kitu ambacho haikuwezekana kufanyika miaka ya zamani.

Anavutiwa jinsi gani makampuni wanatumia uwezo huu wa mtandao kuwafikiwa wateja wao husika kwa njia ambayo inawafanya kuwapenda, kuwaamini na kuwa tayari kununua bidhaa wanazouza.