PUNGUZO YA 80% INAISHA NDANI YA


JINSI YA KUJENGA BIASHARA YA KITAALAMU MTANDAONI

Geuza shs. 500,000 kuwa shs. 3,000,000 Au Zaidi Kila Mwezi Mtandaoni Haraka

Wahi bei ya punguzo kabla haijapanda


Huhitaji Wazo

Mtaji Mdogo

Huhitaji Ujuzi 


Kutoka Mezani kwa Dr. Said Said
Kisauni, Zanzibar
2024
.............................

Mpendwa mjasiriamali wa mtandao mtarajiwa,

Kama unataka kujenga biashara ya kitaalamu mtandaoni inayokuingizia faida ya milioni tatu au zaidi kila mwezi kwa kipindi kifupi... 

Hata kama hauna uzoefu wa biashara na wala haujawahi kuingiza kipato chochote mtandaoni…

Na utapenda kufanya hivyo kwa kwa mtaji mdogo wa hata shs. 500,000…

Basi huenda ujumbe huu ukawa ni ujumbe muhimu kuliko ujumbe wowote katika maisha yako..

Kwanini nasema hivi?

Kwa jina naitwa Dr. Said Said na miaka kadhaa iliyopita nilikuwa sina chochote.

Sikuwa na sehemu ya kuishi wala kipato kinachoeleweka.

Makubwa nilokuwa nayo ni madeni na stress za maisha.

Wenzangu wengi niliomaliza nao chuo walikuwa wameshaajiriwa, wanaingiza vipato vizuri na wameoa na kujenga familia.

Maisha yao yalikuwa yanendelea vizuri.

Japokuwa nilikuwa mhitimu wa stashahada ya udaktari, sikutaka kuajiriwa baada ya kumaliza internship.

Nilitegemea kwa wakati ule kuwa biashara ya Network Marketing niliokuwa nikijenga ingenisaidia kutimiza ndoto zangu.

Lakini WAPI!

Network ilikuwa inakuwa na kubomoka.

Na kipato kilikuwa kinapanda na kushuka.

Hapo ndipo nikaamua kuingia mtandaoni kutafuta mfumo mbadala wa biashara unaofanya kazi…

  • Nilijifunza Web Design na kuwatengenezea watu tovuti (web design agency)
  • Nilijaribu kufanya Drop Shipping
  • Nilifanya Affiliate Marketing
  • Nilijaribu Amazon FBA 
  • Content Marketing pamoja na SEO
  • Google adsense
  • AirBnB
  • Na mengine mengi

Vitu vingi unavyojua vya kutengeneza pesa mtandaoni nilifanya yote.

Badala ya kupata matokeo, muda mwingi nimejikuta nagongesha kichwa changu ukutani kwa tafrani ya kushindwa kufanya hii “biashara ya mtandao” kufanya kazi…

Baadhi ya wakati mafanikio yalikuwa yakininyemelea lakini kabla sijaikamata mkononi, ilikuwa ikiniponyoka... 

...utasema kulikuwa na nguvu ya giza isiyotaka mimi kupata mafanikio. 

Hata kuingiza shs. 500,000 kwa mwezi nilikuwa natumia nguvu kubwa sana. 

Sikuelewa kwanini nilikuwa sipati mafanikio. Nikijianagilia...

  • Vitabu vingi nimesoma
  • Semina kadhaa nimeshahudhuria. 
  • Kuangalia video za Motivation YouTube ndio usiseme 
  • Nishalipia kozi nyingi mtandoani

"Hivi nina kasoro gani mimi?"…

Jambo hili lilikuwa linanikosesha usingizi.  

Kwa vile bado nilikuwa nina njaa ya mafanikio, sikukata tamaa. 

Nikaanza kufuatilia watu wenye mafanikio mtandaoni kutoka marekani pamoja na UK na kuwekeza katika mentorship program zao. 

Moja ya program niliyowekeza ilikuwa kutoka kwa kijana wa UK aliyekuwa akiingiza kipato cha zaidi ya $100,000 kwa wiki kupitia Facebook. 

Baada ya kufanyia kazi program hiyo, nilianza kuona mabadiliko wiki za mwanzo japokuwa yalikuwa mabadiliko madogo. 

Lakini baada ya miezi kadhaa ya kufuatilia wanafunzi wenzangu waliokuwa wakipata mafanikio makubwa, siku moja majibu yaliji download kichwani mwangu kama tofali la tani moja.

Nilikuwa sitoboi kwa sababu ya namna nilivyokuwa nikifikiria kuhusu biashara na namna ya kutengeneza pesa.   

Siku zote nilikuwa nawaza kuwa ninahitaji biashara yenye kulipa peke yake kufanikiwa. 

Japokuwa biashara nzuri ni muhimu kulikuwa na SIRI nyengine 2 ya msingi na ya lazima kuwa nayo kama unataka kupata mafanikio ya hali ya juu haraka. 

Mimi huita mihimili 3 ya biashara. 

Nilivyoanza kufanyia kazi kwa kiasi kidogo tu mambo haya matatu, nilianza kuona mabadiliko chanya. 

Na nilivyomua kuyachukulia serious spidi ya matokeo yaliongezeka kwa kiasi kikubwa mno na maisha yangu yalibadilika kama ifuatayo…

Dr. Said's Story Board
  • Niliweze kufungua ofisi yangu ya kwanza ya kutoa huduma ya Web Design
  • Niliweza kusafiri kwenda Malaysia na Singapore na kukaa zaidi ya mwezi nikiwa mwanafunzi wa chuo
  • Kuoa mke wa ndoto yangu
  • Kuenda Hija
  • na mengine mengi

TUJE LEO

  • Ni muasisi wa kampuni ya Online Profits
  • Ni mshauri wa wafanya biashara (business strategist)
  • Ni mwekezaji katika kampuni ya Afya
  • Na mengine ambayo sitapenda kuyataja

Na tukija kwenye kipato, ni zaidi ya 10 ya kipato cha daktari. 

Mbali na hapo nimeweza kuwasaidia wajasiriamali waliokuwa wakihangaika kutumia formula hii na kupata matokeo kama haya:

Ki ufupi, likija swala la kutengeneza pesa mtandaoni

Alhamdulillah, halinisumbui tena kichwa.

Ninafahamu kwa kiasi kikubwa kitu gani kinafanya kazi na kitu gani hakifanya kazi.

Na cha msingi zaidi:

Ninafahamu kitu gani kinafanya kazi LEO.

Na kwa sasa, natafuta kundi maalum ya watu waliopo SERIOUS wanaotaka kumiliki biashara mtandaoni yenye kuingiza faida ya Milioni 3 au zaidi kwa mwezi ndani ya miezi michache ijayo.

SIRI ILIYONITOA KUWA KIJANA ANAYEHANGAIKA MTAANI HADI KUWA MJASIRIAMALI MASHUHURI MTANDAONI

Sasa unaweza kujiuliza:

Siri gani hiyo niliyogundua iliyosababisha kunitoa kuwa kijana anayehangaika mtaani hadi kuwa mjasiriamali mashuhuri mtandaoni? 

Katika safari yangu ya ujasiriamali, nimegundua kitu…

Miaka yote nipo mtandaoni, watu wengi wamejaribu kuiga vitu nnavyofanya.

  • Wamejaribu kuanzisha agency ya matangazo
  • Wamejaribu kutengeneza kozi kama zangu na kuuza mtandaoni
  • Wamejaribu ku copy na ku paste vitabu vyangu pamoja na content zangu za YouTube
  • N.k.

Lakini mwisho wa siku…

Matokeo ya wengi hayafanani na yangu.

Sasa swali linakuja:

Kama wao wamejaribu kufanya vitu ninavyofanya mbona wanashindwa kupata mafanikio ninayopata?

Kitu gani kinawatofautisha watu wenye mafanikio kama mimi…

...na watu wasio na mafanikio?

Kama wote wanafanya vitu kama mimi ninavyofanya, kwanini wachache mno ndio wanafanikiwa?

MIHIMILI 3 YA BIASHARA YENYE KUHAKIKISHA UNAPATA MAFANIKIO MAKUBWA KWA KIPINDI KIFUPI

Driver - Car - Road

Chukulia safari ya mafanikio ya biashara kama safari ya kutoka mji mmoja kwenda mji mwengine. 

Kufanikisha safari hiyo unahitaji vitu 3:

1. Dereva (Mfanyabiashara)
2. Usafiri (Biashara)
3. Barabara (Strategia)

Bila ya vitu hivyo 3 kamwe hautofika sehemu unayotaka kufika. 

Bahati mbaya watu wengi wana focus katika usafiri peke yake na wanasahau kuhusu dereva na barabara... 

...ndio maana watu hao hupenda kuuliza swali... 

"Biashara gani inalipa?" kabla ya kuuliza, "ninahitaji sifa gani kufanikiwa katika biashara?"

Kuuliza "biashara gani inalipa"  ni sawa na mtu kuuliza "Nimiliki gari gani nikitaka kuelekea Arusha?" hali ya kuwa hajui kuendesha gari.

Kwa hivyo kabla ya ku focus kwenye biashara, elewa kwanza... 

1. Sifa za Mfanyabiashara Mzuri:

Kupata mafanikio mazuri katika biashara unatakiwa kuwa na sifa zifuatazo: 

  1. Clarity: Kuwa na ubayana wa malengo yako (fahamu exactly unataka nini). Unataka kuingiza shs. ngapi kila mwezi? Unataka maisha yako yawe vipi baada ya kuingiza hicho kipato? Je ukiwasha movia ya maisha yako miaka 5 hadi 10 ijayo unaionaje? 
  2. Njaa ya mafanikio: Unatakiwa kuwa na njaa ya mafanikio kuliko mbwa mwitu aliyekuwa hajala chakula mwezi mzima. Kama umeridhika na shida, hustahili mafanikio. 
  3. Kutoogopa Kuchukua Risk: Bila ya kufanya maamuzi katika vitu unavyoogopa kufanya utandelea kusema 'One Day Yes' hadi kuingia kaburini. Amua Sasa na uchukua Risk!
  4. Kupenda Kujifunza: Kuna vitu vingi sana vya kujifunza kwenye biashara yako. Kama wewe mzito wa kujifunza utabaki hapo hapo ulipo. Shida tupu na stress. 
  5. Nidhamu ya Kufa Mtu: Mafanikio makubwa hayatokani na kitu kikubwa unachofanya mara moja bali inatokana na vitu vidogo vidogo unavyofanya kila siku hata kama hujisikii kufanya. Kwa hivyo kama haupo tayari kujenga nidhamu ya kufanya kazi kila siku, biashara sio kwa ajili yako.  

Kama unazo sifa hizo au upo tayari kujenga sifa hizo, sasa unaruhusiwa kuuliza, "biashara gani inalipa?"

Kusema la ukweli biashara nyingi zinalipa ndio kila biashara ina wafanyabiashara wanaofanya vizuri.  

Lakini kuna mfumo fulani wa biashara ambao utakurahisishia kutimiza malengo yako kwa haraka.  

2. Sifa za Biashara Zenye Kulipa:

Tujaalie una shs. 500,000...

...na utapenda laki 5 hiyo izae na kuwa shs. milioni 3 au zaidi kila mwezi. Unafanyaje? 

Una chaguo mbili..

Chaguo la 1: Commodity Business:
Hii ni biashara ya kununua bidhaa (commodity) kwa bei ya chini na kuuza kwa bei ya juu kupata faida.

Watu wengi wanapenda biashara hii kwa sababu ni rahisi kufanya. 

Lakini changamoto zake zinawafanya wengi kukata tamaa na biashara. Changamoto zenyewe ni:

  1. Zinahitaji mitaji mikubwa: Kama lengo ni kuingiza faida ya shs. 3,000,000 au zaidi kila mwezi basi utahitaji kuwa na mtaji mkubwa kufanya hivyo la sivyo itakuchukua kipindi kirefu, tena hapo uombe hujapata washindani. 
  2. Ushindani mkubwa: Kwa vile unauza bidhaa kama wanayouza wengine (labda uzalishe bidhaa ya kipekee mwenyewe), utashindana na wenzako na mtagawana wateja. 
  3. Faida Ndogo: Kwa vile ushindani ni mkubwa, utalazimika kushusha bei kuhakikisha unapata wateja wengi jambo ambalo litasababisha faida kuwa ndogo. 
  4. Ngumu kuikuza: Kama faida ya biashara yako imekuwa ndogo, zoezi la kukuza kipato chako kitakuwa kubwa mno na ndio maana zaidi ya 70% ya biashara ya commodity business hufa ndani ya miaka 2. 

Chaguo la 2: Expert Business

Hii ni aina ya biashara ambayo wateja wako wanakulipa kwa kutatua matatizo yao kupitia utaalamu wako. 

Kwa vile taaluma yako ni kitu kisichoshikika, haikugharamu kila unapotatua matatizo ya kila mteja.  

Biashara hii inafaida zifuatazo: 

  1. Mtaji mdogo: Taaluma yako ndio mtaji wako. Baada ya kujenga taaluma, utaweza kutatua tatizo la kila mteja bila ya kutumia gharama ya ziada; tofauti na commodity business.
  2. Ushindani mdogo: Kwa vile unaingie kwenye soko maalum km. kuwasaidia akina mama waliotoka kujifungua kurudisha shepu zao za mwili, ushindani kwenye masoko kama hayo ni kama hakuna.  
  3. Faida Kubwa: Kama ushindani ni mdogo na unatatua matatizo sokoni vizuri, basi utakuwa na uwezo wa kuwatoza gharama za juu na wao watafurahi kukulipa gharama hizo. Na ukiwa unaingiza shs. 1,000,000 kwa kila mteja na unapata wateja 5 tu kila mwezi, hicho ni kipato cha shs. 5,000,000 kwa mwezi. 
  4. Rahisi Kuikuza: Kwa vile kipato na faida yako ni kubwa unaweza kuwekeza asilimia kubwa ya kipato chako kwenye matangazo ya kulipia jambo ambalo litakuza kipato chako kwa spidi kali mno.

Kwa hivyo umeshaona kuwa expert business ndio biashara ya kufanya. 

Na hata kama unahisi huna taaluma, zipo taaluma nyingi sana ambazo unaweza kujifunza na ndani ya kipindi kifupi ukaweza kuanza kuzifanyia kazi. 

Lakini ufanye biashara gani ya expert business?

Fanya biashara yoyote yenye sifa hizi 4 kama unataka matokeo mazuri:

  1. Iwe Inatatua Tatizo Sugu: Utalipwa pesa nyingi mno kama utaweza kutatua matatizo sugu
  2.  Uwezo Mzuri wa kulipa: Hakikisha unawalenga watu wenye uwezo wa kulipia bidhaa/huduma yako
  3. Soko Lenye Kukua: Hakikisha unalenga soko kubwa au soko linalokuwa. Kaa mbali na masoko yanayoanguka.
  4. Walengwa Wanapatikana Kiurahisi: Hakikisha unaingia kweny soko ambalo ni rahisi kuwafikia walengwa wako hususan mtandaoni.

Baada ya kuwa na sifa ya kuwa mfanyabiashara na kuanzisha biashara ya expert business yenye sifa hizo 4, hatua inayofuata ni kutumia...

3. Stratejia Nzuri ya Kujenga Biashara Yako:

Kuna mifumo 2 unatakiwa kutengeneza kama unataka kuingiza kipato kikubwa haraka: 

1. Mfumo wa kutatua matatizo ya walengwa wako
2. Mashine ya kunasa wateja.

Kwa vile kila biashara inahitaji mfumo wake maalum wa kutatua tatizo, sitozungumzia nukta hiyo hapa.

Kuhusu mashine ya kunasa wateja, huu ni mfumo wa kukusaidia kujenga uaminifu kwa walengwa wako kiurahisi kuweza kufanya mauzo haraka.

Mashine ya Kunasa Wateja

Mashine hii inajengwa kwa kuzingatia hatua tatu:

  1. Traffic
  2. Jukwaa
  3. Mauzo

1:Traffic: 
Hatua ya mwanzo ya mashine ni kununua traffic Facebook, Instagram au Youtube kwa ajili ya kuwafikia walengwa wako.

Unafanya hivyo kwa kubandika matangazo yenye kuzungumzia utatuzi wa matatizo yao.

Kwa mfano kama wewe ni mtaalamu wa kuwasaidia wakurugenzi kutokomeza kitambi na manyama ya uzembe, unaweza kubandika tangazo lenye kichwa cha habari...

"Hatua 3 za Kutokomeza Vitambi na Nyama ya Uzembe Bila ya Kufanya Mazoezi Haraka"

ikisha unawakaribisha katika jukwaa lako...

2: Jukwaa: 
Jukwaa ni sehemu unayowakusanya walengwa wako na kuwafanya wakujue, wakupende na wakuamini.  

Unafanya hivyo kwa kuzungumzia kiundani kuhusu changamoto yao na namna ya kutatua changamoto hiyo (kama mimi ninavyofanya hapa).

Kuna platform tofauti unayoweza kutumia kujenga jukwaa lakini platform inayofanya vizuri ni group la WhatsApp na Email. Ukifanya kazi yako ya kuwaelimisha vizuri basi watakuamini na watapenda kusaidiwa zaidi na wewe.

Hatua ya 3: Mauzo 
Hii ni hatua ya mwisho ya mashine yako. Kama hatua za awali utakuwa umefanya vizuri, kazi iliyobaki ni kuwakaribisha katika ofa ya bidhaa, huduma au program yako. 

Ukiwa unaboresha matangazo yako pamoja na kulipia traffic, ukaboresha na namna unavyoelimisha jukwaa lako itafika wakati utaweza kufanya mauzo ya hadi mara 10 ya pesa unazowekeza kwenye matangazo kama hivi... 

Mashine ya Kunasa Wateja

Hii ndio moja ya sababu kubwa ya wanafunzi wetu kupata matokeo ya ajabu ndani ya kipindi kifupi. 

Sasa swali langu kwako ni je na wewe utapenda kushikwa mkono na sisi kujenga biashara yako kitaamu mtandaoni? 

Kama jibu NDIO basi...

Nakukaribisha katika program ya...

ONLINE PROFITS UNIVERSITY MENTORSHIP

Hii ni program itakayokuongoza kuzindua biashara yako ya kitaalamu mtandaoni, kufanya mauzo ya awali pamoja na kuikuza. 

 Program hii inakuja na:
  1. Kozi ya Wiki 6 ya Online Profits University
  2. Mentorship ya kila wiki pamoja na sapoti
  3. Jumuiya ya wafanyabiashara kama wewe
  4. Live ya kila wiki

Lengo la program ni kukusaidia: 

    1. Kupata Wazo la biashara (kwa mtaji kuanzia laki 5 au zaidi) 
    2. Kuingiza shs. Milioni yako ya mwanzo haraka
    3. Kuikuza na kuvuka shs. Milioni 3, 5 au hata 10 

    Baada ya kujiunga tutakuongoza kama ifuatavyo:

    WIKI YA 1: MSINGI WA BIASHARA

    Wiki hii tuta focus katika kukusaidai kupata wazo la biashara pamoja na kufanya mauzo ya awali. 

    Hapa utajufanza msingi wa biashara na vitu vya kuzingatia kuweza kupata mafanikio kwa urahisi. 

    Baadhi ya vitu tuliyozungumzia ndani ya wiki hii ni kama yafuatayo:

    • Msingi wa biashara: Hapa utafahamu biashara ni kitu gani hasa (watu wengi hawafahamu) na sifa 4 za biashara zenye kulipa.
    • Jinsi ya Kupata Wazo Zuri la Biashara: Hapa tutakupatia mazoezi ya kufanya kupata mawazo 3  mazuri ya biashara. 
    • Jinsi ya Kufanya Mauzo ya Awali: Baada ya hapo tutakufahamisha namna ya ku test wazo lako sokoni hadi kufanya mauzo ya awali kabla ya kuwekeza mtaji wowote katika biashara yako. Kama biashara imekubalika utaendelea nayo. Kama haijakubalika utahamia kwenye wazo jengine.

    WIKI YA 2: ROHO MWILI, AKILI & UTULIVU WA MOYO

    Wiki hii tunakupatia silaha ya kujenga bayana, hali ya kujiamini pamoja na kukupatia formula ya kujenga nidhamu ya kufa mtu. 

    Tutazungumzia nafasi ya roho, mwili pamoja na akili  kuweza kuwa mfanyabiashara usiekamatika. 

    Wiki hii ukiifanyia kazi vizuri utajenga imani ya mafanikio kupindukia.

    Baadhi ya vitu utakayojifunza ni yafuatayo:

    • Jinsi ya kutumia roho yako (soul) kujikurubisha kwa Mola wako, kumtegemea Yeye peke yake uweze kupata mafanikio makubwa pamoja na utulivu wa moyo
    • Sayansi ya kutunza mwili wako kuongeza ufanisi wa kazi
    • Jinsi ya kutumia saikolojia yako kujenga mindset (fikra) na identity ya watu wenye kuingiza vipato vikubwa

    WIKI YA 3: JINSI YA KUJENGA MASHINE YA KUNASA WATEJA

    Baada ya kufanya mauzo ya awali na ushajiande kisaikoljia kufanya mapinduzi, hatua inayofuata ni kujenga mfumo mzuri (mashine) itakayokusaidia kuwafikia walengwa wako, kujenga uaminifu kwao na kuwauzia bidhaa/huduma zako kiurahisi. 

    Wiki hii tutafundisha jinsi ya kujenga huo mfumo.

    Baadhi ya vitu utakavyojifunza ni:

    • Mashine ya kunasa wateja ni kitu gani na namna ya kujenga hiyo mashine
    • Sumaku ya mtandao ni nini na namna ya kutengeneza sumaku ya kuwafanya walengwa wako waache kufanya wanachokifanya na kukusikiliza wewe
    • Namna ya kutumia mfumo wa mahesabu maalum (Financial Tracker) kuweza kuboresha mashine yako iendelee kutema pesa

    WIKI YA 4: MBINU NA SAIKOLOJIA YA KUUZA KAMA WAZIMU

    Wiki hii tunakujenga kuwa bingwa wa kufanya mauzo. 

    Kama mauzo ya awali yalikuwa ni ya kusuasua basi wiki hii utajifunza mbinu zitakazofanya kuuza mtandaoni rahisi kuliko kumsukuma mlevi. 

     Baadhi ya mambo utakayojifunza ni yafuatayo:

    • Jinsi ya kutumia saikolojia ya walengwa wako kufanya mauzo
    • Hatua 7 za kufuata kufanya mauzo kiurahisi
    • Copywritting: Silaha ya kuuza mtandaoni
    • Jinsi ya kusuka ofa ya kufa mtu
    • Jinsi ya kuuza bidhaa za bei ya juu kupitia simu

    Mbali na hayo nitakuzawadia vitabu vifuatavyo BURE kabisa: 

    Jinsi ya Kusuka Ofa ya Kufa Mtu

    Kitabu hiki kitafundisha jinsi ya kusuka OFA za kuwafanya wateja wakubembeleze kununua bidhaa/huduma yako

    Nakala ya Mauzo: Wibul Formula

    Nakala hii ya mauzo itakusaidia kuuza bidhaa za thamani ya shs. 1,000,000 au zaidi kupitia simu

    WIKI YA 5: JINSI YA KUTUMIA FACEBOOK NA INSTAGRAM KUUZA KAMA BINGWA 

    Ukishafahamu namna ya kufanya mauzo vizuri, tutakuonyesha wapi pa kuwapata watu wa kuwauzia

    Wiki hii utajifunza:

    • Jinsi ya kusuka matangazo kama bingwa: Hapa utajifunza formula 4 za kusuka matangazo pamoja na jinsi ya kutumia AI (Artificial Intelligence) kuandika matangazo kama mchawi (formula hii peke yake itakufanya uwe bingwa wa kuandika matangazo ndani ya dakika 5). 
    • Mambo 3 ya kuelewa kabla ya kubandika matangazo
    • Jinsi ya kutumia Facebook Ads Manager kubandika matangazo yanayofanya vizuri
    • Jinsi ya kufunguliwa akaunti ya matangazo iliyofungwa

    Kuhakikisha matangazo yako yatakuwa na mvuto wa hali ya juu, nitakuzawadia kitabu kifuatacho BURE kabisa upate ku copy na ku paste sampuli ya matangazo yangu. 

    Kitabu hichi hakipatikani sehemu nyengine yoyote ile...

    Jinsi ya Kuandika Matangazo Yenye Kunasa Wateja book

    Ndani ya kitabu hiki, nime share formula 9 za kutumia kuweza kuandika matangazo yenye mvuto wa hali ya juu. 

    WIKI YA 6: JINSI YA KUBORESHA NA KUKUZA BIASHARA YAKO

    Hujaridhika na milioni moja kwa mwezi? Usijali 

    Hapa ndipo tutakuonyesha namna ya kukuza biashara yako kuvuka Milioni 3, 5 au hata 10. 

    Jambo la kufurahisha ni kuwa kuingiza Milioni ya pili ni rahisi kuliko milioni ya mwanzo. Na milioni ya 3 ni rahisi kuliko ya 4. 

    Baadhi ya vitu utakavyojifunza ni:

    • Jinsi ya kuokoa muda na kuongeza ufanisi wa biashara yako
    • Jinsi ya kuboresha huduma za biashara yako
    • Jinsi ya kukuza kipato (income scaling)
    • Jinsi ya kurasimisha biashara yako kikamilifu

    Tunaelewa kuwa kila mwanafunzi anajifunza kwa spidi yake na kuna uwezekano usipate matokeo kama ulivyokuwa unategemea ndani ya wiki 6 za mwanzo. 

    Hakuna shida!

    Kuingiza shs. 1,000,000 sio mbio fupi bali ni mbio refu.

    Pengine utapenda kushirikiana na wafanyabiashara wenzako kusaidiana. 

    Usijali. Na ndio maana...

    TUTAKUPATIA TEKNOLOJIA YA KISASA YA SKOOL...!

    Skool Community

    Kijiwe cha Wafanyabiashara

    Utaingizwa katika kijiwe chetu cha skool ambacho kitakufanya ushirikiane na wafanyabiashara wengine. 

    Vile vile utaweza kuuliza maswali, kuona mafanikio ya wanafunzi wengine pamoja na ku share mafanikio yako.  

    Hii ni kama Facebook lakini kwa wafanyabiashara.

    skool classroom

    Access ya Madarasa

    Madarasa yote yapo hewani na unaruhusiwa kuingia muda wowote kutokana na ratiba yako.  Unaenda classroom unabofya open na unapitia mafunzo kwa spidi yako.

    skool classroom
    skool members

    Jenga Mtandao wa Wafanyabiashara

    Kutana na wafanyabiashara wengine wenye ndoto kama zako. Anza kuongea nao na kujenga urafiki. 

    Mara nyengine unayemfahamu ni bora kuliko unachokifahamu. 

    Na chachandu ya ziada...

    TUTAKUZAWADIA NA KOZI ZIFUATAZO BURE KABISA...!

    Siri ya Ujasiri Mockup

    SIRI YA UJASIRI

    (Thamani yake shs. 150,000)

    Unaogopa kuchukua hatua au kufeli? Usijali! Kozi hii fupi itakusaidia kujenga ujasiri wa hali ya juu kuweza kufanya vitu unavyoogopa kufanya.

    AI Magic Mockup

    AI Magic

    (Thamani yake shs. 250,000)

    Unaona umeachwa nyuma? Kozi hii itakuonyesha jinsi ya kutumia teknolojia ya AI kuweza kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu.

    WAHI BEI YA PUNGUZO KABLA BEI KUPANDA

    Chagua Mpango Wako Wa Malipo

    KWA MWAKA

    SHS. 2,500,000 500,000

    Jiunge leo kupatiwa yafuatayo:

    Mentorship ya Online Profits University (AKA Milioni 10 Kwa Mwezi): Hii ni kozi ya wiki 6 pamoja na online mentorship kukusaidia  kujenga biashara ya kitaalamu mtandaono
    Kijiwe cha skool: Hichi ni kijiwe cha kukutana na kushirikiana na wapambanaji wenzako. Hii ni platform kama Facebook lakini kwa wafanyabiashara
    Live ya kila wiki: Tutakana kila wiki live kupatiwa muongozo wa maendeleo yako pamoja na kupatiwa ushauri wa hatua zaa kufuata kutimiza malengo yako 
    Mpango Mkakati kutoka kwa Dr. Said: Dr. Said atakupigia simu na  kukufanyia mpango mkakati wa namna ya kutimiza malengo yako ya kibishara 

    JARIBU MWEZI 1

    SHS. 200,000 50,000

    Jiunge leo kupatiwa yafuatayo:

    Mentorship ya Online Profits University (AKA Milioni 10 Kwa Mwezi): Hii ni kozi ya wiki 6 pamoja na online mentorship kukusaidia  kujenga biashara ya kitaalamu mtandaono
    Kijiwe cha skool: Hichi ni kijiwe cha kukutana na kushirikiana na wapambanaji wenzako. Hii ni platform kama Facebook lakini kwa wafanyabiashara
    Live ya kila wiki: Tutakana kila wiki live kupatiwa muongozo wa maendeleo yako pamoja na kupatiwa ushauri wa hatua zaa kufuata kutimiza malengo yako 

    Jaribu kwa Mwezi 1 kabla ya kulipa kifurushi cha mwaka

    BONUS 

    Program hii inakuja na bonus za jumla ya thamani ya zaidi ya shs. 1,000,000 ambazo utapatiwa BURE kabisa:

    Kozi ya Siri ya Ujasiri: Kozi hii itakusaidia kujenga ujasiri wa kufanya vitu ulivyokuwa unaogopa kufanya (thamani yake shs. 150,000)
    Kozi ya AI Magic: Kozi hii itakufundisha jinsi ya kutumia teknolojia mpya ya Artifitial Intelligence kuongeza ufanisi wa kazi yako (thamani yake shs. 250,000).
    Kitabu cha "Jinsi ya Kuandika Matangazo Yenye Kunasa Wateja": Kitabu hiki kitakufundisha formula 9 za Matangazo zenye kunasa wateja (thamani yake shs. 150,000).
    Kitabu cha: Jinsi ya Kusuka Ofa ya Kufa Mtu: Kitabu hiki kitakufundisha hatua 9 za kufuata kusuka ofa zenye kumfanya mteja atokwe na udenda na kutamani kukupatia pesa kununua bidhaa au huduma yako (thamani yake shs. 150,000)
    Nakala ya Mauzo ya WIBUL: Hii ni nakala ya simu ya mauzo iliyotusaidia kufanya mauzo ya zaidi ya shs. Milioni 200 kupitia simu. (thamani yake shs. 250,000) 
    Nakala ya Mauzo ya 12-Step Formula: Hii ni nakala nyengine ya mauzo tuliokuwa tukitumia kuuza bidhaa za shs. 1,000,000 au zaidi kila mwezi (thamani yake shs. 250,000)

    Maswali na Majibu

    Sina wazo la biashara. Mtanisaidia kupata wazo zuri la biashara?

    Ndio. Ndani ya wiki ya kwanza ya program kuna video kadhaa zitakazokuongoza katika zoezi zima la kujipatia wazo zuri ya biashara inayoendana na personality yako.

    Ninaweza kulipia program lakini sina mtaji wa kutosha wa kuanzisha biashara. Je program itanifaa?

    Kwa vile utakuwa unajenga biashara ya kitaalamu (expert business), mtaji wako ni taaluma yako (expertise) na sio pesa kama ilivyo katika commodity business. Kwa hivyo hauhitaji mtaji mkubwa kujenga biashara yako. 

    Ninahitaji kuwa na elimu gani kupitia program zenu? Mimi ni mhitimu wa darasa la 7.

    Kama unajua kusoma, kuandika na kutumia app kama ya WhatsApp au Instagram basi inatosha sana wewe kuweza kuingia katika program yetu na kufaidika.

    Mimi nina biashara ya Commodity Business. Je hii program itanifaa?

    Kama unataka kukuza commodity business yako hapana. Sikushauri uchukue hii program. Ila kama upo tayari kugeuza biashara yako kuwa ya kitaalamu (expert business) au kuanzisha biashara mpya ya kitaalamu basi program hii itakufaa.

    Ninaweza kulipia kila mwezi badala ya mwaka mzima?

    Hapana. Ila unaweza kulipia mwezi mmoja wa majaribio kabla ya kuamua kulipia mwaka mzima kama utawahi ofa.

    Biashara Yenu Imesajiliwa? Ofisi Zenu Zipo Wapi?

    Ndio! Biashara yetu imesajiliwa na ZBPRA  pamoja na mamlaka za ulipaji kodi ya ZRB pamoja na TRA. Kwa vile biashara yetu ni 100% ya mtandaoni, hatuna ofisi maalum kwa ajili ya kukutana na wateja wetu. Kwa hivyo mauzo yote pamoja na mafundisho na mentorship tunafanya mtandaoni na tumekuwa tukifanya hivyo kwa zaidi ya miaka 5.

    KAMA HUJAPATA MAFANIKIO HADI SASA SIO KOSA LAKO

    Sikiliza, 

    Ninaelewa changamoto yako... 

    Hujaridhika na hali ya maisha yako sasa hivi.

    Na hilo SIO kosa lako. 

    Kila ukiingia YouTube pamoja na mitandao mengine ya kijamii unakutana na mtu mmoja anakwambia kitu kimoja... 

    ...na chapisho linalofuata unakutana na mtu mwengine anaekwambia kitu chengine kinachopingana na mtu wa mwanzo. 

    Mmoja anakwambia biashara inayolipa ni Forex. 

    Mwengine anakwambia hapana ni Network Marketing. 

    Anakuja mwengine anakwambia achana na yote hayo na ufanye cryptocurrency. 

    Kila ukiendelea kuangalia video na kusoma chapisho mpya, badala ya kupata suluhisho ya changamoto yako ndio unazidi kuchanganyikiwa. 

    Ukweli ni kuwa: 

    Unahitaji mentor mmoja mwenye mafanikio akuambie ukweli juu ya hatua unazotakiwa kufuata kutimiza malengo yako. 

    Na ukiingia katika program ya Online Profits University, mimi na makocha wangu tutakwambia ukweli; vitu gani unatakiwa kufanya kujenga biashara ya shs. Milioni 3 au zaidi kila mwezi. 

    SIKILIZA...

    ACHA KUPOTEZA MUDA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

    Watu wengi wanaamini kuwa kuangalia video za motivation na kusoma vitabu vya personal development zitawapatia mafanikio 

    Ukweli ni kwamba: 

    • Huhitaji kuangalia video za wahamasishaji kufanikiwa na wala
    • Huhitaji kusoma vitabu vya personal development kungudua "siri ya mafanikio"

    Unachohitaji ni kitu kimoja pekee...

    Ni kuacha kujilewesha na maarifa za kuhamasisha. 

    Faida za hizi maarifa ni moja tu... 

    ... BURUDANI

    Lakini kama unataka kupata mafanikio ya kudumu acha kupoteza muda kuangalia na kusoma maarifa ...

    ... na uanze kugeuza maarifa uliyokusanya kuwa mchakato wa kutumiza malengo yako hatua kwa hatua. 

    Na ndio maana program yetu ina focus zaidi katika michakato ya kuchukua hatua kuliko kukuburudisha. 

    Hatua za moja kwa moja zitakazokusaidia kuzindua biashara yako na kuingiza shs. 3,000,000 kwa mwezi...

    ...ikiwezekana hata chini ya miezi 4. 

    Na baada ya hapo uweze kutumia formula hiyo tena na tena kupata matokeo makubwa zaidi.

    Mbinu zetu ni rahisi na unaweza kuzifanyia kazi haraka...

    ...kuanzia LEO! 

    Tumeshathibitisha na kuzifanyia majaribio kwetu na kwa wajasiriamali wengi...

    Na uzuri ni kuwa formula utakayojifunza katika program ya Online Profits University inafanya kazi vizuri sana katika soko la mwaka wa 2024. 

    KWANINI TUNAKUPATIA PROGRAM HII KWA BEI YA KUTUPA?

    Ni hivi…

    Kadri unavyosaidia watu wengi, ndivyo unavyopata pesa nyingi.

    Na kwa kuwa nataka kupata pesa nyingi na Online Profits…

    Nahitaji kuwasaidia watu wengi.

    Ndiyo maana maudhui yaliyomo ndani ya program ya Online Profits University yana thamani kubwa ukilinganisha na program nyenginezo zenye kuuzwa Mamilioni.

    Wacha nikuambie ukweli:

    Ninayo program nyengine mtandaoni…

    Program inayozalisha mafanikio makubwa kuliko program yoyote tuliyonayo

    Lakini bahati mbaya hii program inalenga wafanyabiashara wenye kuingiza shs. 3,000,000 au zaidi kila mwezi katika biashara zao. 

    Program hii inawasaidia kukuza biashara zao kuvuka shs. 10,000,000 kwa mwezi.

    Program inaitwa Online Profits Mastermind na inauzwa shs. 6,000,000. 

    Hatuna wanafunzi wengi katika hiyo program lakini ndio inayotuingizia pesa nyingi. 

    Kwa hivyo nikitaka kuingiza kipato kikubwa...

    Sina budi isipokuwa kuwasaidia watu wengi iwezekanavyo kuvuka kipato cha shs. 3,000,000 kwa mwezi waweze kumudu program yangu ya Online Profits Mastermind.

    Na ninafahamu kuwa watu wengi wanaotamani kuwa wanafunzi wangu hawewezi kumudu hiyo program. 

    Ndio maana nimeanzisha program ya Online Profits University kwa bei ya chini.

    Lengo sio kutengeneza pesa NYINGI...

    Bali kuwafikia WATU WENGI...

    Ili tuwasaidie watu wengi iwezekanavyo kuingiza shs. 3,000,000 au zaidi kila mwezi waweze kumudu program yangu ya Online Profits Mastermind.

    Hiyo ndiyo siri iliyopo nyuma ya kuanzishwa kwa program ya Online Profits University

    Wanafunzi Wangu Wengine Wanasemaje...

    Na Wengine Hawa...

    Hujalipia Bado? Unasubiri nini?

    Kumbuka kuwa ofa hii itakapo ondoka itakugharimu shs. 1,000,000 kwa mwaka na hata fursa ya majaribio ya mwezi haitakuwepo tena. Kama utapenda kujiridhisha zaidi kabla ya kufanya malipo nasi kwa kutupigia simu au WhatsApp hapa 0679 536927  

    © Online Profits.  All Rights Reserved.

    mastercard

    Andika Jina, Email & Namba ya Simu

    Tunatumia vielelezo vyako kama tulivyoelekeza katika kurasa ya Privacy Policy. Unaweza kujitoa muda wowote kwa kubofya kitufe cha unsubscribe chini ya email zetu zozote.

    Close

    JINSI YA KUTENGENEZA MASTERCARD NA KUFANYA MALIPO MTANDAONI

    Tengeneza Mastercard na Tigo Pesa

    Tengeneza Mastercard na MPesa

    Tengeneza Mastercard na Airtel Money

    Close