Site icon Online Profits

Jinsi ya kulenga wateja vizuri

Moja ya changamoto ambayo naona wafanyabiashara wengi ninaozungumza nao wanayo ni kutofahamu

njia sahihi ya kulenga wateja wao.  Kama ungependa kujifunza njia sahihi ya kuwalenga wateja wa bidhaa au

huduma unazozitoa basi makala hii ni kwa ajili yako, hivyo isome kwa umakini mkubwa ili uweze kufahamu

kwa undani jinsi ya kuwalenga wateja wako

Kama wewe una biashara na unataka kila mtu awe mteja wako basi una hatari kubwa ya kufeli kwenye

biashara yako. Labda uwe mfanyabishara mkubwa kama Bakhresa ambaye anauza bidhaa za aina

mbalimbali, Lakini kama umeingia katika soko na biashara yako ni changa ni vizuri zaidi ujue mbinu ya

kulenga wateja wako vizuri.

Na mbinu yenyewe ni Kulenga watu wachache badala ya kuhangaika na watu wengi.

 

Kulenga wateja katika biashara yako ni kutafuta sehemu au kundi fulani la watu katika soko na kuamua

kulisaidia kundi hilo. Tuchukulie mfano kwa madaktari wa aina tatu. Daktari wa kwanza awe ni daktari

anayetibu wagonjwa wote (General MD), na daktari wa aina ya pili awe ni daktari anayetibu wagonjwa wa

aina moja tu, mfano anatibu watoto tu, na daktari wa aina ya tatu anatibu ugonjwa fulani tu kwa mfano

daktari anaefanya upasuaji kwa watoto.

 

Kwa haraka haraka unaweza kusema daktari anayetibu magonjwa yote ndiye mwenye mafanikio na

anaingiza pesa nyingi lakini ukweli ni kwamba, Daktari anayetengeneza pesa nyingi zaidi kati ya hawa ni yule

daktari ambaye anatibu wagonjwa wachache zaidi ambaye anafahamika pia kama Daktari bingwa. Kanuni

hiyo inatumika hata katika biashara.

 

Watu wengi wanapoambiwa kutumia mbinu hii ya kuwalenga wateja, wanaona kama watakosa wateja katika

biashara zao. Lakini nakuhakikishia kuwa ukiweza kujiweka katika nafasi kama hiyo ya kulenga wateja wa

aina fulani tu, unaweza kuwavuta wateja husika na watakuwa tayari kukulipa pesa nyingi zaidi ukilinganisha

na kama utataka watu wote wawe wateja wako.

 

Mfano mwingine ni kampuni ya Ferari ambayo inauza idadi ndogo ya magari kwa mwaka lakini

wanatengeneza pesa nyingi kuliko Toyota wanaouza magari mengi kila mwezi. Kwanini?, Sababu ni kwamba

wao wamelenga wateja wachache badala ya kulenga watu wote, hivyo wanaweza kukidhi matakwa ya wateja

wao na wateja wanakuwa tayari kulipa pesa nyingi kwa kuwa wanaridhika na wanachonunua. Hiyo ndiyo

tofauti kati ya kutaka watu wote wawe wateja wako au kutaka watu fulani tu ndio wawe wateja wako. Kwa

hiyo swali ambalo unatakiwa kujiuliza wewe ni, Je unataka kuwa Specialist (mtaalamu) au unataka kujiingiz

a katika ushindani wa kupata wateja wengi. Nasema ni ushindani kwani hauna uhakika kama utapata wateja

wengi. Kama unataka kulenga wateja wachache basi kuna mambo mawili unatakiwa kuwa nayo,

  1. Kwanza Jenga taaluma yako.
  2. Pili, elewa ni kundi gani la watu unataotaka kuwasaidia.

 

Mimi (Dr. Said Said) nilipokuwa nafanya biashara ya Network Marketing nilisema nataka kuwasaidia

wafanyakazi kati ya miaka 35 hadi 45 kuweza kuongeza kipato cha Dollar 1200 kila mwezi kwa kutumia

muda wao wa ziada. Hao ndio watu niliokuwa nawalenga na kila mawasiliano ninayofanya, nikiweka

tangazo, nikiandika makala, nikiandika kitabu, nilikuwa nalenga kundi hilo la watu na wao wakiona meseji

yangu wanaelewa kuwa mimi nilikuwa nawalenga wao.

Hivyo kuanzia leo hakikisha unalenga watu wako vizuri, na hakikisha kuwa bidhaa yako inatatua matatizo ya

walengwa wako.  Jikite katika kutatua matatizo ya wateja wako badala ya kulazimisha kuuza.

 

Ungependa kujifunza zaidi?, Kama jibu ni ndio basi tumekuandalia kozi ambayo utajifunza Jinsi ya Kutumia

Mtandao wa Facebook na Instagram kunasa wateja. Ili kuanza kujifunza kozi hiyo ingia hapa Bonyeza maandishi haya kuanza kusoma

Washirikishe wengine makala hii nzuri ili nao wanufaike nayo kwa kubonyeza vitufe vya mitandao ya kijamii hapo chini.

 

 

Exit mobile version