Kama ulikuwa una ndoto ya kufanya biashara ya mtandao yenye kukupa kipato cha uhakika kila mwezi, wiki au siku lakini ulikuwa hujui pakuanzia, basi tega sikio (au kodoa macho) kwani huenda makala hii ikawa ndio muhimu kuliko makala yoyote utakayosoma mwaka huu.
Katika aya zijajazo utajifunza namna ya kufanya biashara kwenye mtandao wa intaneti yenye kukuingizia kipato chenye kukuwa kila siku.
Ila kabla ya kuendelea naomba nitoe ONYO:
Kama wewe ni dizaini ya mtu mwenye kutafuta njia za mkato kutengeneza pesa bila ya kutaka kufanya jitihada yoyote, nyuzi hii haikuhusu na ninakushauri utoke hapa mara moja.
……
Kama bado upo nina imani kuwa roho yako ipo safi na ni matumaini yangu kuwa upo tayari kujifunza njia za uhakika zitakazoweza kukufanya uwe mjasiriamali wa mtandao mwenye mafanikio.
Hongera sana!
Kwanza kabla sijaendelea inabidi nijibu hili swali ili tuelewane vizuri
Mjasiriamali wa mtandao (Online Entrepreneur) ni mtu wa aina gani?
Kuna tofauti kubwa kati ya kutengeneza pesa kwenye mtandao (make money online) na kujenga biashara ya mtandao (building an online business).
Watu wengi wamefanikiwa kutengeneza pesa kwenye mtandao japokuwa wameshindwa kujenga biashara yenye kudumu na yenye kuwaongezea kipato.
Mwenye kuweza kufanya hivyo ndio tunamuita mjasiriamali wa mtandao (online entrepreneur) ambaye ana taaluma ya kutengeneza na kutumia mifumo (systems) yenye kumsaidia kupata wateja na kujenga biashara yake bila ya kuhangaika kama punda.
Japokuwa kuna biashara aina tofauti kwenye mtandao, mfumo wenye kuleta mafanikio makubwa ni mmoja na ukishaielewa inavyofanya kazi, utaweza kufanya biashara yoyote ile kwenye mtandao na kufanikiwa.
Katika uzi huu nitaongelea zaidi huu mfumo upo vipi na ni jinsi gani unavyoweza kuitumia katika biashara yoyote kupata mafanikio.
Vile vile nitaongelea aina ya biashara (business model) ya mtandao yenye kuwasaidia watu wenye mitaji midogo (chini ya milioni) na kuweza kupata mafanikio makubwa kwa kufuata mfumo wa biashara (business system) nitakaoungelea hivi punde.
Lakini kabla ya kuzungumzia huo mfumo ukoje, tuanze na jambo la msingi kabisa…..
Unatengenezaje Pesa kwenye mtandao?
Utengenezaji wa pesa kwenye mtandao hautofautiani na sehemu nyengine yoyote ile.
Pesa zinatengenezwa baada ya kuuza bidhaa au kutoa huduma inayohitajika kwenye soko.
Bidhaa hizo zinaweza kuwa za kukamatika (physical products) au za dijitali (digital products) kama masomo ya mtandao (e-learning), software n.k.
Huo ndio msingi wa biashara yoyote ile. Iwe ya mtandao (online) au ya mtaani (offline).
Kwa hivyo ukishirikishwa na mtu yoyote kufanya biashara ya mtandao (au yoyote ile) na huduma au bidhaa inayouzwa haipo wazi, mkimbie mtu huyo kama utavyomkimbia shetani.
Je kama huna bidhaa au huduma ya kutoa unaweza kutengeneza pesa?
Kama wewe binafsi huna bidhaa au huduma ya kutoa, unaweza uka promote bidhaa/huduma ya kampuni nyengine na ukalipwa commission.
Mfumo huu unaitwa Affiliate Marketing (ambayo ni tofauti na Network Marketing) na ni mfumo ambao umekuwa maarufu sana na makampuni mengi hata Amazon wanaitoa.
Kuwa affiliate (promoter) unatakiwa kujisajili na baada ya kufanya hivyo, utakabidhiwa linki maalum kwa ajili ya ku promote bidhaa au huduma zao.
Makampuni mengi (kama Amazon) wanakuruhusu kuwa affilate bila ya kununua bidhaa zao ila makampuni mengine (hususan za e-learning) hutoa fursa hiyo kwa wateja wao tu. Na wanafanya hivi kwa sababu hawataki affiliates wao wauze kitu wasichokifahamu.
Mambo Matatu Ya Kufanya Kuweza Kujenga Biashara Kwenye Mtandao:
Kosa kubwa watu wanalofanya baada ya kuwa na bidhaa au kuwa affiliate ni kuingia katika mitandao ya kijamii au forums kama hii na kupromote bidhaa.
Ukifanya hivyo utapata resistance kubwa kwa sababu watu hawakujui, hawakupendi na hawakuamini.
Ili uuze vizuri fuata mfumo ufuatao:
Mfumo wa kujenga biashara kwenye mtandao:
Kuweza kujenga biashara ya uhakika yenye kudumu unatakiwa kuwa na mfumo yenye kulenga katika sehemu hizi tatu:
- Kutengeneza Traffic
- Kujenga jukwaa
- Kufanya mauzo
Kwa kiingereze tunaita 3 C’s of marketing ambayo ni:
- Create Traffic
- Capture Leads
- Convert Sales
1. Kutengeneza Traffic:
Baada ya kuwa na bidhaa au huduma unatakiwa kuhakikisha watu watakaovutika na bidhaa ile wataona ofa zako. Kiufupi unatakiwa kutengeneza traffic kwenye offer yako.
Hili ni jambo ambalo watu wengi wanahangaika nalo japokuwa ni jambo rahisi. Na kinachowafanya wahangaike ni kwa sababu wanatafuta traffic ya bure ambayo ki halisia haipo au ni ngumu mno kuipata.
Kama hununui traffic utajikuta unatumia muda wako mwingi kutafuta traffic na muda ni pesa.
Nishawahi kuliongelea hili kwenye video ifuatayo (ipo kwa kiingereza lakini):
Wataalamu wanashauri uanze na paid traffic.
Na traffic nzuri ya kuanza nayo ni Facebook CPC (Cost Per Click) ambayo unawalipa Facebook kuwalenga watu maalum ambao wanaweza kuhitajia bidhaa au huduma yako.
Lakini kwa vile watu hao hawakutambui sio vyema kutanangaza bidhaa yako bali kujenga ukaribu kwa kuwapa zawadi bure kabisa.
Kwa mfano kama unataka kuuza course kwa wafanyabiashara yenye kuwafundisha namna ya kupata wateja kupitia Facebook, unaweza ukatengeneza video au makala mafupi yenye kichwa cha habari ifuatayo, “Makosa 7 Wafanyabiashara wa Kitanzania Wanafanya Katika Mtandao Wa Facebook“.
Mtu yeyote atakaye bofya tangazo lako anaweza kuwa mteja wa bidhaa zako.
Lipia tangazo lako Facebook na utoe bidhaa hiyo bure ili upate……
2. Kujenga listi ya wateja watarajiwa
Ukilipia tangazo lako hakikisha unapeleka traffic yako katika kurasa yenye kuomba taarifa za mteja wako mtarajiwa.
Kurasa ya namna hiyo huitwa lead capture page na inakuwa ina vitu vifuatavyo:
- Kichwa cha habari yenye kuahidi zawadi kwa wateja wako watarajiwa
- Fomu ya wao kuwacha taarifa zao (hususan barua pepe).
3. Jinsi ya kufanya Mauzo:
Kuna njia mbili ya kufanya mauzo,
- Push Marketing na
- Pull Marketing
Push marketing ni aina ya mauzo ambayo unajaribu kum convince mtu husiku kununua bidha unayouza kila unapowasiliana nae.
Njia hii ndio watu wengi wanayofuata na mafanikio yake ni madogo sana.
Pull marketing ni aina ya marketing ambayo unamuelimisha mteja wako kabla hujaongelea kuhusu bidhaa unayouza.
Wataalam wanasema 90% ya mawasiliano yako kwa listi yako iwe ni kuwaelimisha na 10% iwe ni wewe kuwauzia bidhaa.
Ukifanya hivyo watu kwenye listi yako watakufahamu, watakupenda na watakuamini (know, like and trust you) na kama utafanya kazi yako vizuri, wengine watakuomba uwauzie bidhaa kabla ya wewe kuongelea kuhusu bidhaa yoyote.
Wataalamu wanasema kama utakuwa na listi ya watu na kila siku ukiwatumia barua pepe yenye kuwanufaisha na barua pepe moja kwa wiki yenye kutoa ofa ya bidhaa basi unaweza kutengeneza dola 1 -2 kwa kila mtu aliyekuwemo katika listi yako.
Kwa hivyo kama una listi ya watu 1000 unaweza kutengeneza $1000 hadi $2000 kwa mwezi na kama una listi ya watu 10,000 utakuwa na uwezo wa kutengeneza $10,000 mpaka $20,000 kwa mwezi.
Ndio maana wajasiriamali wa mtandao wana msemo unaosema “The Money Is In The List“.
Baada ya kujenga listi ya wateja watarajiwa, kazi yako kubwa inakuwa kutuma email moja kwa siku.
Je Kama wewe ni mgeni wa mambo hayo, uanze wapi?
Kama unataka kuanza leo kufanya biashara ya uhakika yenye kukuwa kila siku unaweza kufuata hatua zifuatazo:
- Tafuta kampuni yenye kukurusu kuwa Super Affiliate: hizi ni kampuni za affiliate zinazolipa commission kubwa sana. Makampuni haya ni machache na mengi katika haya yanalipa hadi $10,000 kwa kila mauzo.
- Nunua angalau bidhaa moja ya hiyo kampuni upate ku experience.
- Tafuta mfumo (online marketing system) ambayo itakusaidia kuuza na kuelezea bidhaa zako kwa niaba yako. Kuanza kujenga mfumo wako itakuchukuwa muda na utapoteza pesa nyingi kabla hujaanza kuona faida.
- Hakikisha unapata mtu mwenye uzoefu (mentor) akusaidie katika kila hatua ya kukuza biashara yako.
- Msikilize na uchape kazi kama mwendawazimu.
Ofa yangu kwako:
Kama upo serious na una nia ya kuwa mjasiriamali wa mtandao, nipo tayari kukupa muongozo wa bure ikiwa na sifa zifuatazo:
- Unazungumza kiingereza vizuri
- Una internet connection nzuri
- Upo tayari kutumia masaa 2 – 3 kwa siku kujifunza na kujenga biashara yao.
- Una pesa za kuwekeza katika biashara yako na traffic.
- Ni mchapakazi kweli kweli na sio mbabaishaji.
Kama unazo sifa hizo basi bofya hapa ujaze application form.
Nitaipitia form hiyo mimi binafsi na kukupigia simu kwa mahojiano zaidi kabla ya kukukaribisha katika ulimwengu huu wa affiliate marketing.
Nafasi ni chache (napokea wanafunza 5 kila mwezi) na nitakuchagua kwa mujibu wa vipengele 2,
- Sifa zako na
- Kuwahi kwako kufanya application.
Kama una swali lolote, uliza kwa ku comment hapa chini.
Na kama umeona makala hii kuwa ni bomba yenye kupaswa kusambazwa basi fanya hivyo mara moja kwa kubofya Facebook, linkedin au whatsapp.
4 replies to "Jinsi Ya Kuwa Mjasiriamali Wa Mtandao | How To Become an Online Entrepreneur"
Ahsante kwa somo binafsi ninandoto za kufanya biashara ya mtandao japo nakabiliwa na changamoto kubwa mbili a/elimu ya kutosha kuhusiana na bishara hiyo b/ mtaji. Naomba msaada wa mawazo kama itawezekana mh je naweza nikachukua mkopo kwa ajili ya kuanzisha biasha hiyo?? 2.kutokana na uzoefu wako kwenye biashara hii na kulingana na mikopo yetu hii ya ki bongo nitafanikiwa kurudisha mkopo wao kwa wakati?? 3/ Ni mtaji kiasi gani naweza kuanza nao kama mjasiria mali mdogo 4/ Je elim unayotoa ina garama na ni kiasi gan?? na ni kwa njia gani?? Ni hayo tu mkuu ahsante tafadhali naomba muongozo
Kitu cha kwanza ninachoweza kukushauri ni:
1) Wekeza kwenye elimu. Elewa kwanza biashara ya mtandao inaenda vipi,
2) chagua biashara itakayokufaa wewe na ujue manufaa yake kwako itakuwa vipi kwani biashara zipo tofauti na kwenye makala hii nimeongelea moja yao tu.
3) Wekeza pesa ukiwa na dira ya muelekeo gani ya kufuata. Bila ya kufuata hatua 2 za mwanzo kuwekeza pesa haitokusaidia.
Mimi nakushauri ujiunge katika group yetu ya WhatsApp group ambayo tunaelimishana namna ya kufanya biashara ya na kwenye mtandao.
Ni Tsh. 20,000/- kila mwezi. Ukitaka kujiunga bofya kitufe kilichoandikwa ‘wasiliana nasi’ kwenye menu yetu hapo juu.
Dr. Said
Ahsante mkuu
Asante Dr.kwa ambaye kiingereza chake ni chakuunga unga inakuwaje na kwaaliye kuana biashara ya mtandao tayali wanisaidiaje kwa hilo?