Kama umetumia muda mwingi na njia nyingi ili kupata mafanikio lakini umekuwa ukishindwa mara zote,
Soma kwa Umakini mkubwa makala hii kwani huenda ikawa ndio suluhisho pekee la kukusaidia kufikia mafanikiounayoyataka.
Kabla sijakuambia nini cha kufanya ili uweze kuyafikia mafanikio, kwanza nataka ufahamu kwamba kuna kitu
ambacho kinawazuia watu wengi kufikia mafanikio wanayoyataka. Na kitu hicho ni woga. Woga ni hali
inayokuja pale unapotaka kufanya jambo fulani lakini unashindwa kulifanya. Ili kupambana na hali hii
unatakiwa kuwa na uthubutu, hivyo hata kama jambo unaogopa kulifanya wewe lifanye tu kwani
hilo ndilo jambo litakalokufikisha kwenye mafanikio. Ili uweze kuwa na uthubutu huo unatakiwa
kujua Jinsi ya Kuwa Shujaa na Kuyafikia Mafanikio Unayoyataka au “How to use confidence to achieve success”
Kwa hiyo kama haujajijengea mfumo wa kuwa shujaa (kujiamini) katika mambo unayofanya
basi hutopata mafanikio. Kama wewe ni mtu ambaye unaendekeza uwoga, yaani kuna kitu
unashindwa kukifanya na unakubali kubaki katika hali ya kuogopa kwa muda mrefu mpaka inafika wakati hufanyi tena, basi itakuwa ni vigumu kwako kupata mafanikio.
Kama unaona unahangaika siku zote lakini bado haupati mafanikio basi asilimia 90 ya sababu
zinazokuzuia kupata mafanikio ni kuwa wewe haujajenga ushujaa wa kwenda kupambana ili
uweze kufikia mafanikio unayoyataka.
Najua bila shaka unahitaji kujua ili jinsi ya kutoa woga ulionao na kuweka ushujaa
utakaokufanya uweze kufikia mafanikio.
Sasa nifuatilie kwa makini, ili uweze kuondokana na uwoga uliokuwa nao na uweze kujenga
ushujaa utakaokupeleka katika mafanikio unatakiwa uzifanyie kazi fomula tatu zifuatazo.
Fomula ya kwanza ni Courage (Ujasiri)
Hii ni hali au uwezo wa kufanya kitu japokuwa
unaogopa kukifanya. Kwa hivyo kama ulikuwa na ndoto ya
kufanya biashara fulani, basi kitu unachotakiwa kufanya ni kujiuliza hatua ya kwanza
ninayotakiwa kufanya sasa hivi ni kitu gani ili niweze kusogea karibu na ndoto yangu. Kisha
unaanza kufanya japokuwa unaogopa lile jambo. Yaani unakuwa katika hali ya kama anapotokea
jambazi nyumbani kwako na unachukua rungu unaenda kumpiga au kupambana nae japokuwa
unaogopa. Huo ndio ujasiri, fanya hata kama una uwoga.
Ili uweze kujenga confidence, kujiamini au kuwa shujaa ni lazima uende hatua ya pili kwani
kufanya jambo unaloogopa kufanya peke yake haitoshi kukufanya wewe kuwa shujaa,
Ninarudia “Kufanya jambo unaloogopa kufanya peke yake haitoshi kukufanya wewe kuwa
shujaa”. Kwa hiyo hatua/ fomula ya pili ni muhimu sana.
Hatua ya pili (Fomula ya pili) ni Commitment, Kujidhatiti
Baada ya kuamua kuanza
biashara na ukaanzisha biashara huo ni mwanzo na sio mwisho. Kosa kubwa linalofanywa na
wafanyabiashara wengi na kupelekea biashara zao kufa ni kukosa commitment. Commitment ni kujua vitu unavyotakiwa kufanya kila siku na ukaamua kuvifanya hivyo vitu kila siku mpaka ukajenga uzoefu wa kile kitu.
Kwa mfano hivi karibuni nilitoa challenge baada ya mmoja wa wanachama wa kundi la
WhatsApp la Online Profits kuniuliza kwamba nifanye nini ili niweze kupata mafanikio?
. Nikamwambia jenga jukwaa na uwe na commitment ya kuwasiliana na jukwaa lako kila siku.
Na njia nzuri ya kuwasiliana nao ni kurecord video na kuwatumia.
Hatua ya tatu (Fomula ya tatu) ni Capability, Uwezo
Ni kujenga uwezo wa kufanya kitu.
Unataka kupata mafanikio kupitia biashara ni lazima ujenge uwezo wa kuwa mfanyabiashara
mzuri. Unataka kuwa na mafanikio katika riadha basi unatakiwa kujenga uwezo wa kuwa hivyo.
Moja ya kitu unachotakiwa kufanya ili kufikia huko ni kufanya kila siku yaani commitment na
kitu kingine ni kumtafuta mtu mtaalamu, Coach akakushauri juu ya hiko unachotakiwa kufanya.
Kama unataka kuanza biashara ya kuku basi unatakiwa kumtafuta mtaalamu wa biashara ya
kuku akushauri. Pia tafuta vitu unavyotakiwa kufanya kila siku katika biashara ya kuku ili
ufanikiwe na kisha anza kuvifanya.
Kwa hivyo hizo ni fomula tatu za kujenga confidence, kujiamini au kuwa shujaa katika mambo
unayofanya na ukiwa na confidence nakuhakikishia kupata mafanikio kwako ni lazima.
Kama ungependa kujifunza jinsi ya kutumia mtandao wa facebook na instagram kunasa wateja basi tumeandaa kozi nzuri sana kwa ajili yako. Bofya link hii uanze kusoma Bonyeza hapa kuingia Darasani.
Usisahau kuwashirikisha wengine katika mitandao ya kijamii kwa kubonyeza kitufe hapo chini. Na kama una maoni andika katika sehemu ya comment,