Kama wewe ni mfanyabiashara na umeanzisha page yako ya biashara na moja ya malengo yako ni kupata

likes nyingi kwa mfano kupata likes laki 1 au milioni basi nakuhakikihshia kuwa hiyo ni stretejia mbaya katika

biashara yako na utakuwa hauna tofauti na mtu mwenye likes tano. Najua jambo hili linaweza kuwashangaza

wengi.

 

Ni hivi, mwishoni mwa mwaka 2017 Mark Zuckerberg alitangaza kuwa kuna mabadiliko yatafanywa katika

facebook 2018 na mabadiliko hayo yataathiri wamiliki wa kurasa za Facebook.  Ili kuelewa mabadiliko hayo,

tutaelezea facebook ni nini? Zamani Facebook ilivyoanza ilikuwa inawaunganisha watu yaani ndugu, jamaa

na marafiki. Ulikuwa ni mtandao uliojikita sana kijamii na sio kibiashara. Hivyo facebook ilipata umaarufu

mkubwa na watumiaji wengi zaidi. Baadae makampuni nayo yalifikiria jinsi gani wanaweza kutumia facebook

ili kuwaunganisha na wateja wao.

 

Ndipo Facebook walipoamua kuanzisha Facebook Page (Ukurasa Wa Facebook). Hivyo watu wanao-like

page wanaweza kuona matukio yanayowekwa kwenye Kurasa walizozipenda. Kwa hiyo kila unavyokuwa na

likes nyingi ndivyo posts za page yako zinavyoonekana na watu wengi zaidi. Na hiyo ilisababisha kila

anayetengeneza page/kurasa atumie muda mwingi na nguvu kubwa katika kuhakikisha kuwa anapata likes

nyingi kwani likes nyingi zinaashiria kuwa matangazo ya kurasa yako yataonekana na watu wengi.

 

Baadae Facebook walianzisha Boosting (Mfumo wa kulipa matangazo ya facebook), na hivyo walipunguza

idadi ya watu wanaoweza kuona matangazo ya kurasa (organic reach). Ilikuwa ni kwa wastani wa 7% ya

jumla ya watu waliopenda kurasa yako ndiyo wanaoweza kuona tangazo au post uliyoweka katika Kurasa ya

Facebook. Hivyo kwa mfano kama Kurasa yako ya facebook ina likes 1,000,000 (milioni), ni watu 70,000 elfu

70 tu ndio wanaweza kuona post yako na weliobaki laki 9 hawaoni.

 

Mwishoni mwa mwaka jana (2017), Mark Zuckerberg alitangaza pia kuwa mwaka huu watapunguza zaidi

idadi ya watu kuona matangazo yasiyolipiwa katika page hata kama wame-like page hiyo. Mfano unaweza

kuwa na page yenye likes 1,000,000 (milioni moja) lakini ukiweka tangazo linaweza kuonekana na watu

wachache zaidi au lisionekane kabisa na hata mtu mmoja.

 

Kwa hiyo sasa hivi kupata likes nyingi sio stretejia nzuri. Kupata likes nyingi kunachukua muda mrefu na

utatakiwa kupost mara kwa mara hadi watu wakujue na bado haina tija yoyote. Stretejia nzuri sasa hivi ni

kufanya boosting (kulipia matangazo). Ukitumia mfumo huu wa kulipia matangazo, matangazo yako

yataonekana na watu wengi hata kama katika page yako hakuna mtu aliye-like.

Wafanyabiashara wadogo wanaweza wakaona kuwa mfumo huu utawarudisha nyuma, lakini ukweli ni

kwamba njia hii ndio yenye tija zaidi katika kutangaza facebook.

Kama unataka kujifunza namna ya kufanya page advertising (Boosting) kupitia facebook, basi tumeandaa

kozi inayoitwa Facebook-Insta Course. Kuanza kusoma kozi hiyo Bofya hapa

Kama una swali lolote usisite kuuliza kupitia comments

Imeandaliwa na Dr. Said Said , CEO – Online Profits

Imehaririwa na Abdallah Hemedi, Content Manager – Online Profits


Abdallah Hemedi
Abdallah Hemedi

Content Manager

Ujumbe Wa Facebook

Leave a Reply

Your email address will not be published.