Katika mafunzo yetu ya leo tutazungumzia Mambo matatu ya msingi na ya muhimu unayotakiwa kuyafanya
katika mtandao ili uweze kupata wateja kwa wingi na kwa kiingereza tunaita mambo haya matatu “The three C’s of Marketing”.
C ya kwanza ni Create traffic: Unatakiwa kuonekana mbele ya macho ya watu wengi. Kuna tofauti kubwa
kama watakuona watu 10 kwa siku na watu 1000 kwa siku, Ni wazi kabisa kwamba wakikuona watu wengi
mauzo nayo yatakuwa mengi zaidi. Ukishatengeneza traffic hautangazi bidhaa unazouza au huduma
unazotoa bali unatangaza SUMAKU. Sumaku ni zawadi ambayo unaitangaza kwa wateja wako watarajiwa.
Kwa mfano kama unataka kuuza cream za kuondoa chunusi usoni badala ya kutangaza cream yako,
unawaambia Kama una tatizo la chunusi la muda mrefu basi nimeandaa Group ya WhatsApp ambayo
inafundisha namna ya kuondoa chunusi sugu ndani ya siku tatu kama unataka kujifunza karibu katika group
yetu na andika namba yako chini. Hiyo ndiyo Sumaku na ndio maana unawanasa watu.
C ya pili ni Capture Leads: Katika hatua hii tunakusanya taarifa zao Jina, namba ya simu na email. Na
ukishapata taarifa zao unaanza kuwasiliana nao kupitia jukwaa lako. Katika kuwasiliana nao unatakiwa
kujenga uaminifu, unajenga ukaribu kwao na unawafundisha ili kujenga trust. Na ukishafanya hivyo ndio
tunakuja kwenye C ya mwisho.
C ya tatu ni Convert sales: Hatua hii ndio unatangaza bidhaa au huduma unazotoa. Mwisho unaweza
kuwaambia kama nilivyosema katika mafunzo ya leo tumeona kuwa zipo cream maalumu ambazo zinaweza
kuondoa chunusi ndani ya muda mfupi. Na cream ambazo na nakushauri utumie ni cream za aina fulani.
Kama ungependa kupata hii cream unaweza kunijulisha na pia utambue kuwa cream zilizobaki ni chache na
ukichukua cream sasa hivi nitakupa na bonus ya kitu . Hapa unaonyesha kuwa una nia safi ya kumsaidia. Na
kama unayo ofa mpe ofa kwa sababu huyo mteja hajawahi kununua kabla kutoka kwako. Kwa hiyo ni vizuri
mauzo ya kwanza ukatoa na ofa au Discount (punguzo la bei), kufanya hivyo itakusaidia sana kuuza.
Kwa hiyo mambo matatu ya kufanya katika mtandao ili kupata wateja kwa wingi ni Create traffic- hapa
unaweza kutumia facebook au instagram kwa kulipia matangazo kwa kuwalenga watu husika unaowahitaji
kama vijana, wanawake au wakurugenzi wa kampuni. Pili unakusanya taarifa zao na mwisho unafanya
mauzo.
Kama una swali au maoni juu ya makala hii basi acha comment yako na usisahau kuwashirikisha wengine ili nao wanufaike na mafunzo haya mazuri na muhimu sana kwao kwa kubonyeza vitufe vya mitandao ya kijamii hapo chini.