Kama una biashara na unafikiria kuikuza biashara yako kwa muda mrefu kuanzia miaka mitano hadi kumi basi makala hii ni kwa ajili yako. Mambo ya msingi unayotakiwa kuyazingatia ili uweze kuikuza biashara yako ni:-

1.Traffic: Traffic ni uwezo wa kuwa mbele ya macho ya watu wengi. Kama una bidhaa au huduma nzuri lakini huwezi kuwepo mbele ya macho ya watu wengi basi utapata shida sana kuuza bidhaa au huduma unayotoa.  Kama huna ujuzi wa kutengeneza traffic utaangaika sana katika kukuza biashara yako kwenye mtandao. Traffic inapatikana kwa kutafuta sehemu ambayo ina watu wengi na wewe unajiweka hapo.

 

Mfano wa sehemu zenye watu wengi katika mtandao ni Facebook ambayo ina watumiaji billioni 1.5, Instagram ambayo ina watumiaji Milioni 800 na sehemu nyingine ni Google ambayo ina watumiaji wengi sana kuliko tovuti nyingine yoyote duniani. Pia zipo hata website za ndani ya nchi kama JamiiForums ni sehemu unayoweza kupata traffic kwa ajili ya kutangaza bidhaa au huduma unayotoa.

 

2.Kuwa na mfumo wa kuweza kunasa wateja kwenye mtandao au kwa jina lingine ni Sumaku ya Mtandao ambayo pia kwa kiingereza inajulikana kama Online Marketing Funnel. Ni muhimu kuwa na Sumaku ya mtandao. Huu ni mfumo ambao baada ya kuitoa traffic unaipeleka katika mfumo ambao unamchukua mtu hatua moja hadi hatua nyingine mpaka anakuja kuwa mteja wako.

Ni lazima ufahamu mteja hatoi maamuzi ya kununua papo hapo, ni lazima kuna vitu vinatakiwa vitokee hatua kwa hatua kabla ya yeye kununua.

Mimi [Dr. Said] Mfumo wa kunasa wateja ndiyo kitu pekee kilichonipa mafanikio makubwa sana katika biashara yangu kuliko kitu kingine chochote. Watu wengi wakiniona mara ya kwanza huwa hawanijui, hawanipendi na hawaniamini, lakini kwa vile nawaingiza kwenye mfumo nawatoa hatua moja kwenda hatua nyingine na hadi wanafikia katika hatua ya kuwa wateja baada ya kunijua, kunipenda na kuniamini.

 

  1. Branding. Hili ni jambo muhimu sana katika biashara yako. Siku zote huwa nawaambia watu “Play the long game”, Cheza mchezo mrefu, msiwe na haraka. Weka malengo ya muda mrefu kwamba baada ya miaka mitano nitakuwa wapi. Mhasisi wa mtandao wa Amazon Jeff Bezos anasema “brand ni maneno ambayo mteja wako anakuzungumzia wakati wewe haupo.” Wewe ukiwa mbali mteja wako anakuonaje? Japokuwa wengine wanataka waonekane kuwa wana bidhaa bora na wanawajali wateja wao lakini wanavyojibrand katika soko haiendani na uhalisi wa brand yao.

Mimi napenda watu wafocus katika kujenga brand, yaani ujenge jina katika soko. Watu hawanunui bidhaa bali wananunua brand. Makala itakayofuata tutaeleza kwa undani kuhusu branding.

Pia tumekuandalia video nzuri, Ndani ya video hiyo utajifunza Jinsi ya Kutumia Mtandao wa Facebook na Instagram Kunasa Wateja. Kuangalia video hiyo Bofya hapa

 

Kama umejifunza kitu comment na kama una swali usisite kuuliza. Usisahau kuwashirikisha wengine nmakala hii kwa kubonyeza vitufe vya mitandao ya kijamii hapo jini.

Dr Said, CEO Online Profits


Abdallah Hemedi
Abdallah Hemedi

Content Manager

Ujumbe Wa Facebook

Leave a Reply

Your email address will not be published.