Hatua 1: Jiandae kisaikolojia
Ndani ya eneo hili tutazungumzia kuhusu mambo ya kujiandaa nayo kisaikolojia ili kuweza kufanikisha malengo yako kama kujijengea nidhamu yako ya kila siku, siri ya mafanikio, kuondoa uoga, kujijengea ujasiri n.k
1 - Mambo 3 ya kufanya kila siku
Muda wa Video: 14:26
Ndani ya video hii mkufunzi wako Dr. Said ataanza kukuelezea ni mambo gani matatu unayotakiwa kufanya kila siku ili kuweza kujiandaa vizuri kisaikolojia kupata mafanikio.
1b - Jinzi ya kutumia Google Calendar Kwenye Simu
Muda wa Video: 8:23
Ndani ya video hii utapata kuelewa jinsi ya kutumia Google calendar kupangilia ratiba yako ya kila siku kama tasks, events za kuhushuria nakadhalika
2 - Siri ya Mafanikio
Muda wa Video: 7:45
Ndani ya video hii utapata kuelekezwa ni jinsi gani watu wenye mafanikio kwenye biashara zako wanavyoweza kufikia malengo yao. Siri ni
1: Wana Clarity ya Hali ya Juu
2: Wana Imani isiyotetereka kuhusu uwezo wao wa kutimiza malengo yao
3: Wamejenga Nidhamu ya kufanya vitu vyenye kuwapelekea kwenye Mafanikio
3 - Ndoto ya Bruce Lee ya Kuingiza $10 Million
Muda wa Video: 18:26
Ndani ya video hii utapata kuelekezwa ndoto ya Bruce Lee ya kuingiza $10 Million kwa muda maalum aliouwena, kuwa na Chuo cha Kong Fu na alievyoeleza jinsi atatekeleza na kufaikiwa malengo yake.
4: Jinsi ya Kudanganya Ubongo Kunasa Mafanikio
Muda wa Video: 19:45
Ndani ya video hii utapata kuelekezwa jinsi ya kupata mafanikio ya baadae kwa kuudanganya ubongo wako kuamini kwamba unaweza bila ya kijiwekea vikwazo.
5- Kuhusu Kitabu Cha The One Thing
Muda wa Video: 7:13
Ndani ya video hii utapata kujua mambo yalioyomo kitabu cha The One Thing-By Garry Keller.
6: Mduara wa Mafanikio
Muda wa Video: 12:15
Ndani ya video hii utapata kuelezewa kuhusu ramani ya mafanikio. Vipi utaweza kujitengezea ramani itakayoweza kukusaidia kufikia malengo yako ya mwaka au miaka mitatu ya baadae.
Kujiwekea Malengo, kujijengea mazoea na kuwa na imani na unacho kifanya.
7: Kwanini Watu Hawatimizi Malengo Yao
Muda wa Video: 3:16
Ndani ya video hii utapata kuelezewa Kwa nini watu wengi wanashindwa kutimiza malengo yao na wapi wanapokosea.
8: Ikigai Yako ni Nini?
Muda wa Video: 15:16
Ndani ya video hii utapata kuelezewa Kuhusu falsafa ya Kijapani iitwayo IKIGAI. Falsafa hii ama fomula ni ile ambayo ukiigundua unaweza kupata mafanikio makubwa. kufanya jambo ambalo unaweza kulifanya kwa ubora zaidi na kwa mapenzi
Zoezi:
Install WhatsApp business katika simu yako na fanya setup
9: Tumia Ikigai Yako Kuandaa Lengo Kubwa
Muda wa Video: 15:16
Ndani ya video hii utapata kuelezewa Kuhusu kutumia IKIGAI yako kuandaa lengo kuu.
10a: 411 na Malengo ya Utendaji Kazi
Muda wa Video: 10:44
Ndani ya Video hii utaelezwa jinsi ya kujipangaia malengo yako ya kiutendaji kazi ya kila siku, mwaka mmoja baadae na miaka mitano ijayo.
10b: 411 na Malengo ya Utendaji Kazi
Muda wa Video: 10:44
Ndani ya Video hii utaelezwa kwa undani zaidi jinsi ya kujipangaia malengo yako ya kiutendaji kazi ya kila siku, mwaka mmoja baadae na miaka mitano ijayo.
Zoezi:
1. Malengo unayotaka kutimiza ndani ya siku moja
Download Hii Document Kufanya mazoezi kama ilivyoelekezwa kwenye Video.
11: Jinsi ya Kujenga Nidhamu ya Mafanikio
Muda wa Video: 10:44
Ndani ya Video hii utaelezwa jinsi ya kujenga nidhamu ya kujenga mafanikio katika biashara yako.
Kujijengea mambo ya msingi unayotakiwa kufanya KILA SIKU.
kujenga mazoea ya kufanya jambo 1 kati ya hayo kila siku kwa siku 66 zijazo hadi iwe mazoea
12: Jenga Identity Mpya
Muda wa Video: 10:44 Ndani ya Video hii utaelezwa kwa undani jinsi gani ya kujijengea Identity mpya na ya kupata mafanikio katika biashara yako
Zoezi:
1. Andika list ya identity unayotaka kujenga
2. Itangaze - watu unaowaamini
3. Anza kuzifanyia kazi - Focus na identity moja tu - The One Thing - 66 days
13: Pambana na Uoga na Jenga Ujasiri
Muda wa Video: 10:44 Ndani ya Video hii utaelezwaChanzo cha Uoga, jinsi ya kupambana na uoga na jinsi ya kujenga ujasiri.
14: Muhtasari
Muda wa Video: 10:44Ndani ya Video hii utaelezwa kwa Muhsatari jinsi ya kujiiandae Kisaikolojia Kuingizia Faida ya Milioni Kwa Mwezi.