Kama wewe ni mfanyakazi au mfanyabiashara na haijalishi unafanya biashara gani, aidha
unafanya Network Marketing, au Una duka lako unauza nguo au wewe ni Daktari au ni Mhandisi (Engineer),
au kazi yoyote nyingine unayofanya basi nifuatilie kwa makini sana katika makala hii. Kwani ninaenda
kukuonyesha jambo muhimu sana kwako. Kabla sijakuambia jambo hilo angalia tatizo kubwa lililopo katika jamii.
Tatizo kubwa ninaloliona katika jamii ni kuwa watu wengi wanataka kujifunza mambo mengi
badala ya kujifunza mambo machache na kuzama ndani juu ya mambo hayo machache na huenda wewe
unayesoma makala hii ukawa mmojawapo.
Bruce Lee aliwahi kusema “Simwogopi mtu aliyejifunza mateke elfu kumi bali
namwogopa mtu ambaye amejifunza teke moja mara elfu kumi”. Kwa nini alisema hivyo?,
Sababu ni kwamba mtu aliyejifunza teke moja mara elfu kumi anakuwa amemaster kile kitu kuliko mtu yoyote.
Siku hizi tuna vyanzo vingi vya taarifa na maarifa, idadi kubwa ya watu wanasoma vitabu vingi
lakini wanachokijua katika wanayoyasoma ni maarifa machache tu ya juu juu na sio kwa undani.
Kama unataka kuzama ndani katika kile unachokisoma basi unatakiwa uchukue taarifa uliyoisoma,
uiweke katika utekelezaji na unaifanyia mazoezi, unaijaribu katika soko mpaka unakuwa
mtaalamu wa kile kitu, na hili ndilo jambo ambalo limekosekana kwa wafanyabiashara wengi.
Unaweza kukutana na mtu ambaye amesoma vitabu vya Success (Mafanikio) lakini anahangaika, kwa nini?,
Sababu ni kwamba anakusanya maarifa mengi badala ya kufocus taarifa chache ambazo atazifahamu kwa
undani na kuzifanyia kazi.
Mfano mzuri kuna kitabu kinaitwa Think and Grow Rich, Kitabu hiki kinasemekana ndio kitabu
kilichozalisha matajiri wengi Duniani kuliko kitabu kingine chochote, kama umesoma hiki kitabu
na hakuna hatua uliyopiga katika maisha yako, na ukasoma kitabu kingine labda umesoma Rich
Dad, Poor Dad na haujapiga hatua katika maisha yako na ukasoma kitabu kingine labda How To
Win Friends and Influence People na bado haujapiga hatua yoyote katika maisha yako, hapo
unatakiwa upunguze kusoma vitabu na uchague kitabu kimoja na uchukue kile kitabu uhakikishe
unapiga hatua kupitia hicho kitabu na usonge mbele mpaka uone kitabu hiki kimeshanifikisha
mpaka hapa sasa nahitaji kitabu kingine.
Na njia nzuri ya kukusanya taarifa niliyojifunza ni kwamba ujue kwanza unataka nini, na una
malengo gani? Na uamue unataka kumaster kitu gani, kwa mfano unataka kuwa mtaalamu katika
Facebook Marketing, Kwa hivyo jambo la kwanza ni kujiuliza kuna vitabu gani vinavyohusu
Facebook Marketing ninavyotakiwa kusoma na hutakiwi kusoma kitabu kingine chochote
isipokuwa kinachohusu Facebook Marketing, hapo ndio unazama katika Marketing. Swali la pili
ni nani anayefanya Facebook Marketing anifundishe au niweze kununua kozi yake, nani atakuwa
Mentor (Mshauri) atakayeniongoza katika masuala ya Facebook Marketing kwa hiyo hapo
unazama ndani zaidi katika topic moja. Ukishafikia hatua ambayo umeridhika katika Facebook
Marketing na unataka kwenda hatua nyingine basi tafuta taarifa ambayo itakupeleka katika hatua
nyingine. Tatizo ninaloliona kwa watu ni kusoma taarifa nyingi kwa wakati mmoja bila kuzifanyia
kazi. Unakuta mtu anasoma Facebook Marketing, muda huohuo anasoma Bitcoin, muda huohuo
anasoma Investing (Uwekezaji), anasoma Success, akili yake inamdanganya kuwa anafanya kitu
sahihi lakini si hivyo bali anajiumiza mwenyewe.
Najua wengi wanaweza wasipende kuambiwa ukweli huo lakini huo ndio uhalisia. Kwa hiyo
jambo la muhimu ni kuzama zaidi katika jambo moja badala ya kuhangaika na mengi.
Pia kama ungependa kutumia mtandao wa Facebook na Instagram kunasa wateja kama sumaku, basi tumeandaa kozi ya nzuri kwa ajili yako. Kuanza kusoma Kozi hiyo Bofya Hapa