Baada ya kuona wafanyabiashara katika nchi tofauti ikiwemo India, Brazil na nchi zenye kuendelea wakitumia

WhatsApp kuwasiliana na wateja wao, whatsApp wameamua kuzindua app yao ya biashara.

App hiyo ilizinduliwa mwezi wa Septemba mwaka jana nchini Brazil, India na Marekani na mwaka huu kuizindua dunia nzima.

Kama wewe ni mfanyabiashara na unatumia namba mbili za simu, moja yako binafsi na nyengine kwa ajili ya

biashara basi utafaidika sana na App hii kwani utaweza kutumia app zote mbili kwenye simu yako.

Haya ndio maneno waliozungumza Whatsapp kwenye blog yao.

Watu  duniani kote wanatumia WhatsApp kuungana na biashara ndogondogo ambazo wana maslahi nazo kuanzia makampuni ya nguo India  mpaka store za vifaa vya vyombo vya moto Brazil.

Lakini WhatsApp iliundwa kwa ajili ya watu na tunataka kuiboresha iwe ya kibiashara zaidi. Kwa mfano, kwa kuifanya iwe ni rahisi kwa biashara kuwajibu wateja, kutenganisha kati ya messages za wateja na messages za watu wa kawaida na kujenga uwepo rasmi wa mtandaoni.

Hivyo  tunairusha WhatsApp kwa ajili ya Biashara –ikiwa ni bure kabisa kuipakua katika Play Store kwa ajili ya biashara ndogondogo.

App yetu mpya itayarahisishia makampuni kuungana na wateja wao na ni rafiki sana kwa watumiaji wetu wapatao bilioni 1.3  kuwasiliana na biashara wanazofanya nazo kazi..

 

Jinsi  WhatsApp  ya Biashara inavyofanya Kazi

Wasifu wa Biashara: Hii itawasaidia watumiaji wenye taarifa muhimu kama Maelezo mafupi ya Biashara zao, Baruapepe, Anuani na Tovuti.

Nyenzo za Ujumbe: Okoa muda kwa nyenzo bomba za ujumbe ikiwemo- Majbu ya haraka ambayo hutoa

majibu ya haraka kwa maswali yanayoulizwa sana, Jumbe za Salamu zinazowatambulisha wateja wako

kuhusu biashara yako, Na Jumbe za Kutokuwepo ambazo zinawafahamisha wateja wako kuwa sasa una

shughuli nyingine.

Takwimu za Jumbe: Hii inakuwezesha kujua taarifa zaidi za jumbe(messages) unazotuma ikiwemo na zimesomwa na watu wangapi.

WhatsApp ya Mtandaoni: Tuma na pokea jumbe (messages) kupitia WhatsApp ya Mtandaoni katika Kompyuta Yako.

Aina ya Akaunti: Watu watajua kuwa wanazungumza na Biashara kwa sababu utaorodheshwa kama

Akaunti ya Biashara. Baada ya muda baadhi ya biashara zitakuwa na akaunti zilizothibitishwa hivyo. Baada ya

kuthibitishwa namba ya simu ya akaunti inaendana na ile ya biashara.

Na watu wataendelea kuwa na utwala kamili  katika jumbe wanazopokea, wakiwa na uwezo wa kublock

namba yoyote ikiwemo na ya biashara na kutoa taarifa ya baruataka(spam).

“Asilimia 80 ya biashara ndogondogo India na Brazil wanasema WhatsApp inawasaidia kuwasiliana na wateja

na kukuza biashara zao. Na hivyo WhatsApp ya Biashara itarahisisha zaidi katika kuwaunganisha wateja na

biashara.”

 


Abdallah Hemedi
Abdallah Hemedi

Content Manager

Ujumbe Wa Facebook

Leave a Reply

Your email address will not be published.