Kama unamiliki biashara lakini haina kurasa ya Facebook hakikisha unafungua kurasa yako SASA HIVI kwa kufuata utaratibu nilioandika kwenye makala ya Jinsi Ya Kuanzisha Kuarasa ya Biashara Kwenye Mtandao Wa Facebook. Ukishamaliza rudi hapa ujifunze jinsi ya kupata wafuasi 1000 au zaidi ndani ya siku 10.

Kama tayari unayo kurasa ya biashara kwenye mtandao wa Facebook lakini hupati wateja kutokana na uhaba wa wafuasi katika kurasa hiyo, basi hakikisha unaisoma makala hii kwa makini sana.

Pata Makala Yako Ya Masoko Facebook Bure

Ndani ya dakika chache zijazo utajifunza utaratibu ambao wataalamu wa Facebook wametumia kupata wafuasi 1000 au zaidi katika kurasa zao za Facebook ndani ya siku 10.

Mimi binafsi nilifanikiwa kunasa wafuasi zaidi ya 1000 ndani ya wiki moja katika kurasa 3 ninazomiliki nilipoanza kutumia utaratibu nitakaokuonesha hivi punde. Kurasa ninazoziongelea hapa ni:

  1. Kurasa ya Online Profits yenye wafuasi 4,609Online Profits Facebook Page
    Kurasa hii tulivyoianzisha miaka michache iliyopita ilikuwa kwa kasi na kufikia ukubwa wa wafuasi 2,668 kwa siku chache sana.

    Angalia grafu na ujumbe niliowatumia wafuasi wetu hapo chini:online profits fast growth

    Na tumekuwa tukitumia formula hiyo hiyo kutoka kuwa na wafuasi 1000 mpaka 2000 kama uonavyo hapa chini.
    2000 fan member

  2. Kurasa Ya LeoWapi yenye wafuasi 1,508leowapi facebook page

  3. Kurasa Ya SaidSaid yenye wafuasi 4,573Dr.SaidSaid Facebook Page

Cha kufurahisha ni kuwa kupata wafuasi 1000 au zaidi ni rahisi sana kiasi ambacho utatamani ungelijua kufanya hivyo miaka mingi iliyopita jambo ambalo lingekusaidia kuweza kunasa wateja mara kwa mara kwenye biashara yako.

Na jambo la kufurahisha zaidi ni kuwa ukitaka kuongeza wafuasi kutoka 1000 kwenda 2000 au zaidi, unaweza kufanya hivyo bila ya hata kujikuna kicha.

Kama Kupata Wafuasi Kwenye Kurasa Ya Facebook Ni Rahisi Mbona Wengi Hawawezi?

Japokuwa ni rahisi sana kupata wafuasi, kuna mambo mawili yanayowakwamisha baadhi ya wamiliki wa kurasa za Facebook.

Na mambo hayo ni . . . . .

  1. Ukosefu wa Taaluma Hiyo na . . . . . 
  2. Kutowekeza PESA. 

Japokuwa ni jambo rahisi sana kupata wafuasi wengi kwa haraka katika kurasa yako ya Facebook, utahitajika kuwekeza pesa. Kama wewe ni mfanyabiashara wa ukweli, hutokuwa na hofu kuwekeza pesa.

Lakini usijali.

Nina habari nzuri. . . . .

Ukifuata utaratibu nitakaokuonesha hivi punde hatua kwa hatua, utaweza ukapata wafuasi 1000 au zaidi ndani ya wiki kwa gharama isiyozidi $20.

. . . . .Ambayo ni sawa na kupata wafuasi 50 kwa kila $1. 

Na kama biashara (au tovuti) yako itahitaji wafuasi wengi kama 10,000 basi bajeti ya kati ya $80 mpaka $150 inatosha kabisa.

Lakini kabla sijakuonyesha jinsi ya kupata wafuasi hao, unatakiwa kukaa mkao wa kupokea wafuasi wako kwa kufanya yafuatayo:

  1. Hakikisha kurasa umeitengeneza vizuri kiasi ambacho watizamaji wa kurasa hiyo wanapata kutambua kurasa yako ndani ya sekunde 5 inahusu nini na watafaidika vipi:Kufanya hivyo inabidi uwe na(i) Picha ndogo yenye nembo ya biashara yako,
    (ii) Picha ya ukutani yenye mvuto na yenye ujumbe wa kueleweka
    (iii) Jina na maelezo ya waziAngalia mifano ya kurasa hizi hapa upate kuelewa ninamaanisha nini:

    1. Coca Cola:
      kurasa ya coca cola
    2. Kurasa Ya Starbucks:
      kurasa ya starbucksUwe unawasiliana na wafuasi wako angalau mara 2 kwa siku kwa:
      (i) Kuwafurahisha
      (ii)Kuwaelimisha na
      (ii)Kuwapa MotishaUsitumie mtandao wa Facebook kuuza bidhaa au huduma zao isipokuwa kwa nadra sana. Facebook sio sehemu ya kuuza bidhaa. Facebook ni sehemu ya kujenga mahusiano na wateja wako watarajiwa. Na unatumia mtandao huo kuwavutia ili wapate kutembelea tovuti yako ambayo utatumia stratejia maalum kwa ajili ya kuuza bidhaa na huduma unazotoa jambo ambalo ni somo la siku nyengine.Mifano ya taarifa zenye kufurahisha, kuelimisha na kutoa motisha ni kama zifuatazo:

      1. Picha yenye ujumbe mzito (au wa kufurahisha):Money Doesn't Make You Happy
      2. Picha yenye kuchekesha
        funny photo post with laptops
      3. Video yenye kuelimisha
        video ya kuelimisha
        Baada ya kufanya hayo, utakuwa tayari kupokea wafuasi 1000 au zaidi ndani ya wiki moja.
  2. Hatua inayofuata ni kuwaalika marafiki zako kwenye page yako kwa kufuata hatua ziufatazo:
    1.  Fungua kurasa yako na ubofye invite friends to like this page (kama unatumia Facebook kwa lugha ya kiswahili tafuta maneno yaliyoandikwa waalike marafiki wapende ukurusa huu)
      invite friends to like this page
    2. Baada ya kubofya utaona marafiki zako wakijitokeza. Aanza kuwaalika mmoja mmoja kupenda kurasa yako kwa kubofya invite (Alika):
      invite friends to like your page
      Kama una marafiki 500 au zaidi kwenye Facebook yako binafsi na ukawaalika wote, basi unaweza kupata watu 100 au zaidi ku like kurasa yako mara moja. Na kama utakuwa umeshaanza ku post vitu kwenye ukuta wako wenye kuwaelimisha, kuwafurahisha na kuwachekesha wengine wataanza kuzipenda na mpaka kuzisambaza kitu ambacho kitawafanya watu wengine (ambao si wafuasi wa kurasa yako) ku like au ku comment.
  3. Pitia taarifa zote ulizoziweka kwenye ukuta wako na kuangalia nani ame like, comment na ku share. Waalike na wao kwa kufanya hivi:
    1. Bofya sehemu walio like ujembe wako:
      Click those who liked your post
    2. Bofya invite (Alika) kwa wote waliokuwa hawaja like kurasa yako:
      click invite
  4. Kinachofuata sasa ni kubadilisha gia kwenda gia namba nne kwa kutangaza kurasa yako ya biashara upate kuwafikia watu wengi.Kama utakuwa umefuata utaratibu vizuri kama nilivyoelekeza hapo awali basi unaweza kupata wafuasi 1000 au zaidi kwa siku kwa $20 pekee.(NB: Gharama hizi ni kwa kurasa ambazo zinalenga soko la Tanzania. Gharama huwa juu katika nchi za magharibi ambazo masoko yana ushindani mkubwa).Fanya hivyo kwa kubofya Promote Page (Tangaza Ukurasa):
    promote pageBaada ya kubofya utaona kitu kama hiki:
    promote page Fuata hatua ifuatayo kuhakikisha watu wako watarajiwa wanavutiwa na ku like kurasa yako:

    1. Bofya EDIT kwenye AD CREATIVE (kama unavyoona kwenye picha ya hapo juu):
    2. Rekebisha ujumbe unaotaka wenye kuona matangazo waone. Hakikisha unawajulisha unafanya nini na wao watafaidika vipi kutoka kwako.Mimi nimeandika ujumbe huu:“Tunawasaidia wafanyabiashara kunasa wateja kama smaku kwenye mtandao. Bofya Like”ad message
      Kama unataka kubadilisha picha unaweza kufanya hivyo kwa kubofya Upload na kuweka picha nyengine yenye mvuto.
    3. Nenda kwenye Audience uchague jinsia (sex), umri (age) na mji unaotaka tangazo lako lionekane. Mimi nimechagua jinsia zote, umri kati ya 25 – 65 (huu ndio umri ya wafanyabiashara wengi Tanzania) na nimelenga tangazo langu lionekane Tanzania peke yake kama unavyoona hapa chini:
      Ad - audience
    4. Hatua hii ni moja ya hatua muhimu sana kwani hapa ndipo pa kuwalenga watu husika wenye hamu na bidhaa au huduma unazotoa. Usipofanya hivyo utajikuta unapata wafuasi wengi waliokuwa hawapo tayari kununua chochote kutoka kwako.Katika Interest (mapendeleo) chagua watu wenye kupenda vitu vinavyoendana na bidhaa / huduma unazotoa. Kwa mfano sisi (Online Profits) tunalenga makampuni yenye hamu ya kupata wateja kupitia mtandao. Nimechagua sifa kama Advertising (Matangazo), Mass Media, Public Relations, Sales Promotion, Online Advertising, Display Advertising.Ni bora zaidi kupata likes chache zenye thamani kuliko nyingi zilizokuwa hazina thamani.Ad - interests
    5. Hatua inayofuata ni kuweka bajeti ya tangazo lako na idadi ya siku unazotaka tangazo lako lionekane. Bajeti ya chini kabisa ni $5 / siku. Kama una nia ya kupata wafuasi wengi kwa haraka unaweza kuweka bajeti ya $10 / siku.Katika tangazo langu, Facebook wananipa makisio ya kupata likes kati ya 60 hadi 240 kwa siku kwa bajeti ya $5 (ambayo ni likes nyingi sana kwa gharama hiyo) kama uonavyo hapa chini:budget - duration
      chagua idadi ya siku unazotaka kuweka. Kama kurasa yako ni mpya mimi nakushauri uanze angalau na siku 7.Ukifuata utaratibu wote niliokufahamisha katika makala hii unaweza kupata likes 250 au zaidi kwa siku ambayo ni 1750 ndani ya wiki moja.Na kama utakuwa unawaelimisha, unawafurahisha na kuwapa motisha wafuasi wako, hizo likes zitazidi maradufu na hatimae kuwapata baadhi yao kuwa wateja wako wa kudumu.

    6. Hatua ya mwisho ni kuchagu mfumo wa malipo na kulipia tangazo lako. Facebook wanapokea mifumo miwili ya malipo; kadi ya credit/debit (VISA au MASTER) na Paypal.
      Kama hujawahi kufanya malipo kwenye mtandao usishtuke. Hili jambo lishakuwa la kawaida na mabenki mengi ikiwemo CRDB, EXIM, NBC, Standard Charted na mengineo wanatoa hizo huduma. Kama una haraka na unataka kuweka matangazo leo na huna kadi unaweza kuelekea ABC Bank na kujisajili na kadi ya Visa Travel Money. Huhitaji kuwa na akounti na wanakukabidhi kadi yako papo kwa hapo na baada ya masaa machache utaweza kufanya malipo kwenye mtandao.

      Andika vielelezo vyako vya kadi na ubofye Promote:
      promote your Facebook Page

Safi sana. Ushafanikiwa kuweka tangazo lako.
Tangazo lako litaonekana kama hivi:

Kwenye Kompyuta:
tangazo kwenye kompyuta

Kwenye Simu:
Tangazo kwenye simu

Hongera!

Kama umefuata na wewe utaratibu niliokupa hatua kwa hatua kupata wafuasi 1000 au zaidi ndani ya wiki moja litakuwa ni jambo rahisi kuliko kumsukuma mwizi.

Kama utakutana na changamoto usisite kunijulisha kwa kuniaandikia ujumbe hapo chini.

Kama umefaidika na makala hii naomba unisaidie kuisambaza kwa marafiki zako wa Facebook kwa kubofya Poa (like) hapo chini.  Na kama ungependa kujifunza jinsi gani ya kuwafanya wafuasi wako kuwa wateja wako, shusha kitabu cha Masoko Facebook kwa kubofya hapa.Pata Makala Yako Ya Masoko Facebook Bure

Wako, mwenye kujali mafanikio yako

Dr. Said Said

Oh! Kabla sijasahau,

Si umeona kuwa kurasa ya Online Profits ilikuwa na wafuasi 4609 hapo juu nilipoanza kuandika makala?

Namalizia makala hii siku ya pili na wafuasi wameongezeka na kufikia 5353. Watu 744 wameongezeka ndani ya siku mbili na nimetumia $10 tu ambayo ni sawa na wafuasi 74 kwa kila $1.

Facebook growth
Ok! Mimi naondoka.

Tutaonana kwenye makala mengine

 


Ujumbe Wa Facebook

Leave a Reply

Your email address will not be published.