Kama una biashara na unataka kujifunza kutumia Facebook na Instagram kunasa wateja basi bofya hapa kuangalia video kujifunza “Jinsi Ya Kutumia Mtandao wa Facebook na Instagram Kunasa Wateja
Kama umeshawahi kufanya matangazo kwenye mtandao wa Facebook au Instagram na kuambulia patupu basi ukifuata formula hii ya 4 M utaona mafanikio makubwa kuliko njia nyengine yoyote utakayotumia.
Formula hii sikuivumbua mimi bali nimeipata kutoka kwa mtaalamu mmoja kutoka Canada aitwae Nicholas Kusmich anayesifika kuzalisha pesa nyingi kwa makampuni tofauti kupitia mtandao wa Facebook kuliko mtu mwengine yoyote yule duniani.

Na ameweza kufanya hivyo sio kwa sababu anajua kusuka matangazo mazuri kuliko mtu yeyote bali anatumia formula ya 4M na vile vile kuelewa saikolojia ya jamii (Social Psychology) kuliko watangazaji na wanamasoko wengi.
Kwa hivyo formula ya 4 M ni nini?
4 M ni vitu vinne vinavyoanza na herufi ya M.

1: Market (Soko)

M ya kwanza ni Market yaani, soko lako.
Kabla ya kufanya tangazo lako kwenye Facebook au Instagram ni muhimu sana kutambua soko lako.
Wateja wako ni nani?
  • Wako wapi?
  • Wana umri gani?
  • Wanasumbuliwa na kitu gani?
  • Wanatumia mitandao gani ya kijamii?
  • n.k
Kila ukiifahamu soko lako vizuri ndivyo itakuwa rahisi kuwalenga na kuwafikia kupitia Facebook na Instagram.
Uzuri wa Facebook na Instagram ni kuwa ina takwimu za kutosha kukusaidia kuwalenga wateja wako watarajiwa kuliko mitandao mengine yote ya kijamii.
Kosa kubwa wanalofanya wafanyabiashara ni kuhisi kuwa kila mtu yumo kwenye soko lake.
Seth Godin mtaalamu wa masoko anasema,
“Everybody is NOT your market.”
yaani,
Kila mtu sio soko lako.”
Hata kama unahisi bidhaa yako inaweza kupendwa na kila mtu, ni kundi la watu wachache watakaovutiwa na bidhaa zako zaidi ya wengine.
Kwa mfano kama unauza jezi za mpira, utakuta ni vijana wa kiume kati ya miaka 18 hadi 35 ndio wenye kununua hizo jezi kuliko kila makundi mengine ya watu.
Vijana hao ni zaidi ya 70% ya soko lako.
Na kama unataka kuuza jezi za Real Madrid lenga watu wanaopenda kurasa ya Facebook ya Real Madrid au wenye kuwa follow Real Madrid kwenye Instagram.
Ukifanya hivyo matangazo yako yatakuwa bei nafuu kwani umewalenga watu husika.

2: Magnet (Smaku)

M ya pili ni Smaku.
Hili ni jambo ambalo wengi wetu hatulifahamu lakini ni jambo ambalo litakuleta matunda makubwa kwenye kutangaza Facebook na Instagram kuliko jambo lolote.
Wajasiriamali wengi huwa wanakimbilia kuweka picha na maelezo ya bidhaa yao kwenye Facebook na Instagram na kutangaza kuwa bidhaa zao ni nzuri na wawatafute kupata hiyo bidhaa.
Mara nyingi ukifanya hivyo, hutoona matunda mazuri kwa sababu zifuatazo:
  1. Facebook na Instagram haikutengenezwa kwa lengo la kutangaza bidhaa kwa watu.
  2. Na hakuna anayeingia Facebook kwa lengo la kuona matangazo ya watu.
Wanaingia ku:
  1. Socialize‘ (jumuika) na wenzao
  2. kuchat na marafiki zao
  3. kuangalia mapya yaliyojiri kwa watu wanaowafuata.
  4. Kujifunza mambo mapya kupitia video na makala zinazosambazwa na watu
  5. Na wengine kama mimi kupata hapari mpya (hatununui magazeti wala kuangalia habari kwenye TV)
Kama tangazo lako halifanyi lolote kati ya hayo mambo 5 basi kwa mara nyingi litakuwa linachukiwa na watu na halitozaa matunda mazuri.

Smaku ni nini na kwanini unatakiwa kuwa nayo?

Smaku ni zawadi unayowapa wateja wako watarajiwa kwa malengo ya:
  1. Kuwafahamu wateja wako watarajiwa ni kina nani
  2. Kujenga mahusiano mazuri kwao
  3. Kujiweka kwenye soko kama mtaalamu wa kutatua matatizo waliyonayo
  4. Kujenga uaminifu kwao
  5. Kukusanya taarifa zao (yaani majina, email na/au namba zao za simu)
Kwa mfano kama unataka kuuza cream ya kuondoa chunusi usoni unaweza kufanya hivyo kwa kuanza kutangaza kijijaridu kifupi ulichokiandika chenye kichwa cha habari…
“Jinsi Ya Kuondoa Chunusi Sugu Usoni Mwako Ndani ya Siku 3 Kwa Kufuata Hatua 5 Hizi… “
Na ukawagawa jarida hilo kwao BURE kabisa kwa njia ya elektroniki.
Ukifanya hivyo watafurahi, watakupenda na wataona kuwa kweli unania ya kuwasaidia jambo ambalo litakusaidia kujenga uaminifu kwa haraka.
Kwa hivyo kila mwenye tatizo la kuwa na chunusi sugu (au hata lisilokuwa sugu) watataka kupata nakala ya jarida lako hilo.
Najua hadi sasa utakuwa na swali hili kichwani…
Lakini Dr. Said, nikifanya hivyo nitauza vipi bidhaa zangu?
Njia kwanza ya kuuza bidhaa zako ni kuweka kipengele mwisho wa jarida kuwashauri (kwa vile ulikuwa unawaelisha, wanakuona kama mshauri wao na sio mmachinga anayekimbilia kuuza kutengeneza pesa kwenye mauzo) kununua bidhaa yenye kututua tatizo lao.
Hakikisha 80% hadi 90% ya jarida lako linawaelimisha wateja wako watarajiwa na 10% hadi 20% unatumia kuzungzia kuhusu kwa nini wanahitaji kuwa na bidhaa yako.
Njia ya pili ya kuuza bidhaa zako ni kutumia jukwaa lako (email) kuwapa maelezo ya bidhaa/huduma unazotoa. Utaona zaidia kuhusu hili katika M ya 4.
Smaku yako inaweza ikawa kwa mifumo ifuatayo:
  1. Kijijaridu kifupi
  2. Darasa bure (webinar) kama mfano niliotumia mie hapo chini
  3. Video yenye kuelimisha
  4. Bidhaa ya kugawa bure. NB: Hakikisha bidhaa unayotoa ina mahusiano na bidhaa unayotaka kuwauzia. (Kwa mfano kama wewe ni fundi wa iPhone na unataka kuwajua wamiliki wa iPhone unaweza kutoa cover za iPhone bure au kama unauza suti unaweza kutoa vifungo maalum za mashati ya suti cufflinks bure).

3: Message (Ujumbe)

M ya 3 ni Message (ujumbe).
Wengi vile vile wanakosea katika kuandika ujumbe wa matangazo yao.
Wanazungumzia sana kuhusu bidhaa/huduma wanayotoa badala ya kuzungumzia matatizo ya wateja wao watarajiwa na kuwaahidi namna ya kutatua matatizo hayo.
Nimekoleza neno kuwaahadi kwa sababu tangazo linatakiwa kutoa ahadi ya kutatua tatizo la wateja wako watarajiwa na sio kuuza bidhaa (isipokuwa kwa kesi maalum).
Ngoja nikuonyeshe mfano:
Hili ni moja ya tangazo lilopokewa vizuri sana na watu.
Kwa $14 tumeweza kukusanya taarifa (majina na email) za watu zaidi ya 200.
Tangazo hili lilionekana Facebook na Instagram na tulikuwa tunawakaribisha watu kuhudhuria darasa live lenye kufundisha “Jinsi Ya Kutumia Mtandao Kunasa Wateja Kama Smaku
Hebu tulichambue hili tangazo:
Kipengele cha kwanza:
Je wewe ni mfanyabiashara au mjasirimali unaehangaika kupata wateja kupitia mtandao?
Kama unavyoona, nimeanza na swali linalolowagusa wateja wangu watarajiwa.
Kama anayesoma si mhusika, sina mpango nae.
Kipengele cha pili:
Kama ndio basi usihofu kwani Dr. Said Said, Mkurugenzi wa kampuni ya Online Profits ameandaa darasa bure kwenye mtandao ambayo utajifunza “Jinsi ya kutumia mtandao wa intaneti kunasa wateja kama SMAKU
Ikisha nimejaribu kujenga uaminifu kwa kujitambulisha kwa jina na cheo changu.
Kipengele hiki ni muhimu kwani inawaonyesha wateja wako wewe ni nani na kwanini wanatakiwa kukusikiliza.
Kipengele cha tatu:
Katika darasa hili utagundua yafuatayo:
 
1. Kwa nini wajasiriamali wengi wanashindwa kupata wateja kupitia mtandao
2. Siri ya kupata wateja wengi wenye hamu ya kununua bidhaa au huduma unayotoa
3. Mfumo wa mtandao pekee wenye uhakika wa kukuletea wateja wengi kuliko kitu chochote
Nimewaambia watapata nini wakibofya linki.
Kumbuka, lengo ni kutoa sio kuuza.
Kipengele cha nne:
 
Muda unakimbia na siti ni chache.
 
Jisajili sasa hivi kwa kuenda hapa>> https://goo.gl/rMc3Lk
Nimewapa linki na kuwahimiza kwanini wanatakiwa kuchukua hatua mara moja na kutosubiri baadae.
Bila ya kufanya hivyo wapo watakaopuuza na kusema nitafanya baadae.
Na formula hiyo huwa naitumia takriban katika matangazo yangu yote.
Kama unataka kujifunza kiundani hatua kwa hatua nimeenda wapi kwenye mtandao wa Facebook kuandaa hilo tangazo, unaweza kusoma makala ya “Jinsi Ya Kutangaza na Kupata Wateja Wengi Kupitia Mtandao Wa Facebook

4: Mechanism (Mfumo)

Wajasiriamali wengi wanaoweka matangazo kwenye Facebook au Instagram hawafuati mfumo wowote.
Kama unataka kuuza bidhaa/huduma nyingi kwenye mtandao na kutumia pesa kidogo, basi kuwa na mfumo ni jambo usiloweza kujiepusha nalo.
Lakini kabla sijaelezea kuhusu mfumo nataka kwanza nibadilishe mtazamo wako kuhusu matangazo.
Wengi wetu tumejengwa na nadharia ya kutangaza kwa lengo la kuuza bidhaa / huduma zetu.
Lakini kama nilivyokuonyesha, majukwaa ya Facebook na Instagram sio mazuri kwa kutangaza bidhaa au huduma unazotoa (isipokuwa kwa kesi maalum).
Kwa hivyo, cha kufanya ni kujenga jukwaa lako litakalokuruhusu kufanya hivyo bila ya kuwakera watu.
Kwa hivyo badala ya kutangaza kuhusu bidhaa zako kwenye majukwa ya Facebook na Instagram, unawatoa katika majukwa hayo na kuwapeleka katika jukwaa lako (ambayo ni email).
Tumia Facebook na Instagram kwa lengo la kukusanya taarifa za wateja wako watarajiwa, na sio kuuza bidhaa / huduma unazotoa.
Ila usifanye kama 95% ya watu wanavyofanya kutuma maelfu ya email kutangaza bidhaa zako tu.
Ukifanya hivyo utawakera watu na watu wataingiza email zako kwenye spam.
Tumia 80% hadi 90% ya email kuwaelimisha na kujenga ukaribu kwao na 10% hadi 20% kutangaza bidhaa/huduma zako.
Wataalamu wa mtandao wanasema kuwa,
Kwa mteja mpya kununua bidhaa kutoka kwake unahitaji kuwasiliana nae si chini ya mara 7.
Na kwa vile facebook wanakukata pesa kwa kila watu wanavyoona matangazo yako, hutoweza kumudu kutangaza mara 7 kwa watu wale wale.
Lakini kama utakusanya email za wateja wako watarajiwa, utakuwa na uwezo wa kuwasiliana nao mara kwa mara bila ya kutumia gharama yoyote ya ziada.
Kwa hivyo formula ya kufuata ni kama yafuatayo:
Kujifunza zaidi kuhusu mfumo wa kupata wateja kwenye mtandao unaweza kuangalia video ya darasa langu nililofanya live “Jinsi ya Kutumia Mtandao Kunasa Wateja Kama Smaku” hapa.
Hizo ndizo M 4 za kufuata kupata mafanikio makubwa kwenye Facebook na Instagram:
  1. Market (Soko)
  2. Magnet (Smaku)
  3. Message (Ujumbe)
  4. Mechanism (Mfumo)
Kama umependa makala hii basi utapenda video niliokuandalia yenye kukuonyesha “Jinsi ya Kutumia Mtandao wa Facebook na Instagram Kunasa Wateja
Tafadhali nisaidie kusambaza makala hii ili na wengine wafaidike.
Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako,
Dr. Said Said
CEO Online Profits

Ujumbe Wa Facebook

Leave a Reply

Your email address will not be published.