Kama unayo kurasa ya biashara kwenye mtandao wa Faebook na ungependa kupata wateja kupitia mtandao huo, shusha kitabu cha Masoko Facebook BURE hapa.

Sio siri kuwa Facebook inatawala ulimwengu wa mtandao.

Mtandao huo una watumiaji zaidi ya Bilioni 1.4 (idadi kubwa kuliko ya watu wanaoishi Uchina) kwa mwezi na kila mtumiaji anatumia wastani wa dakika 20 kwa siku.

Kwa lugha nyengine, 20% ya muda wote unaotumiwa kwenye mtandao unatumika katika mtandao wa Facebook. [Chanzo: Business Insider]

Na kwa vile biashara yako inahitaji kuonekana mbele ya watu wengi, basi huna budi isipokuwa kufungua kurasa ya biashara yako katika mtandao huo (Facebook Fan Page) na nitakuonyesha hatua kwa hatua jinsi gani ya kufanya hivyo.

Kufanya hivyo unahitaji kwanza kuwa mwanachama wa Facebook. Kama bado hujajisajili na mtandao huo, unaweza kufanya hivyo kwa kuenda Facebook.Com.

Baada ya hapo utaweza kusajili kurasa ya biashara ya Facebook kwa kufuata hatua zifuatayo:

 1. Nenda https://www.facebook.com/pages/create.Hakikisha kurasa hiyo ipo kwa lugha ya kiswahili (kama kiingereza kinakupa shida) kwa kuenda chini kabisa ya kurasa na bofya linki iliyoandikwa English.
  link-english
  Baada ya hapo tafuta lugha ya kiswahili na ubofye:
  kiswahili
  Baada ya kufanya hivyo unatakiwa kuona kurasa yako imebadilika lugha kutoka kiingereza na kuwa katika lugha ya kiswahili kama uonavyo hapa:
  kurasa ya biashara facebook
 2. Chagua aina ya kurasa ya biashara unayotaka kutengeneza kati ya hizo sita zilizoorodheshwa.Mimi nitasajili kurasa yangu kwa kuchagua (kwa kubofya) Kampuni, Shirika Au Taasisi na nitachagua huduma za kupata ushauri/biashara kama kitengo cha biashara yangu. Wewe chagua inayokuhusu.
  Kurasa-Facebook-Chagua-kitengo
 3. Baada ya hapo andika jina la kampuni yako (mimi nimetumia jina la Biashara Consultants kama mfano) ikisha bofya Anza.Kurasa Ya Biashara Jina La Biashara
 4. Sanidi kurasa yako kwa kufuata hatua na maelekezo utakayopewa na Facebook.
  Sanidi Kurasa Ya Facebook
 5. Ukishamaliza bofya Hifadhi Maelezo na tayari utakuwa una kurasa yako ya biashara.

Kama utakuwa umefuata maelekezo vizuri, utakuwa na kurasa ya biashara yako ilikamilika yenye vitu vifuatayo:

Online Profits Kurasa Ya Facebook Ya Biashara

 1. Picha kubwa ya mvuto yenye kuelezea bidhaa au kampuni yako
 2. Picha ndogo yenye Logo ya kampuni yako
 3. Vielelezo vyako vya biashara yako kama:
  1. Wewe ni nani
  2. unapatikana wapi
  3. Mawasiliano yako
 4. Maelezo kuhusu huduma unazotoa.
 5. Kitufe cha kuwasiliana na wewe kitakachowapeleka kwenye mtandao wako

Ukishafanya hivyo utakuwa tayari kupata wafuasi kwenye kurasa yako na watakuwa wakipata taarifa mbali mbali kutoka kwenye kurasa hiyo.

Natumai umenufaika na makala hii.

Kama bado huna kurasa yako ya biashara ya Facebook, basi fanya hivyo mara moja na utujuze kwa ku comment hapo chini.

Pata Makala Yako Ya Masoko Facebook Bure

Na kama una swali lolote usisite vile vile kutuuliza.

Na muhimu zaidi kuliko yote, usisahau kubofya poa na kusambaza makala hii kwa marafiki zako.

Tutaonana kwenye makala menggine ijayo.

Ni mimi mpenda mafanikio yako,

Dr. Said Said


Ujumbe Wa Facebook

  1 Response to "Jinsi Ya Kuanzisha Kurasa Ya Biashara Kwenye Mtandao Wa Facebook"

Leave a Reply

Your email address will not be published.