Wafanyabiashara na wajasiriamali wengi hujishughulisha kutafuta wateja wapya wakiona kipato chao hakikidhi malengo yao.

Kama mwezi uliopita aliingiza kipato cha miliona 1 kutokana na wateja 100, mwezi unaofuata hupanga mikakati ya kutafuta wateja 100 wengine kupata milioni 2 jambo ambalo sio rahisi na lenye kugharimu pesa (za matangazo).

Mbaya zaidi ni pale gharama za kupata hao wateja 100 wapya zikawa zinakaribia au hata kufikia kipato cha wateja 100 hao.

Wateja wanakuwa wengi na faida inakuwa haijaongezeka.

Je kuna njia iliyobora ya kuongeza kipato zaidi ya hiyo ya kutafuta wateja wapya?

Japokuwa kufanya hivyo ni muhimu sana, kuna njia ya rahisi na ya haraka ya kuongeza kipato isiyohitaji wewe kutafuta wateja wapya.

Njia yenyewe ni….

Njia Rahisi na ya Haraka ya Kuongeza Kipato

Wafanyabiashara wengi hawafahamu kuwa kuna njia rahisi na haraka ya kuongeza kipato na njia yenyewe ni…

Kuongeza mauzo kwa kila mteja

Ninamaanisha nini?

Kama umeingiza miliona 1 mwezi ulopita kutokana na wateja 100, inamaanisha unatengeneza wastani wa shilingi 10,000 kutoka kwa kila mteja.

Na kama 10,000 hiyo inatokana na bidhaa/huduma moja, ukiongeza bidhaa/huduma nyengine ya 10,000 inayoendana na bidhaa ile ya mwanzo basi kipato chako kitazidi mara mbili kutokana na idadi ile ile ya wateja.

Kwa hivyo badala ya kutengeneza Milioni moja utakuwa umetengeneza Milioni 2 bila kugharamia matangazo.

Swala la kujiuliza ni…

Je, wateja wangu watapenda kuwa na bidhaa gani pamoja na bidhaa ninayowapa?

Kama unafanya biashara ya kutengeneza tovuti, unaweza ukaongeza huduma zifuatazo:

  1. Usajili wa tovuti (domain name registration)
  2. Urushaji wa tovuti (web hosting)
  3. Utengenezaji wa logo (logo design)
  4. Utengenezaji wa business card
  5. Kuhakikisha tovuti yake inaonekana kwenye Google (Search Engine Optimization)
  6. Kuhakikisha anajenga listi ya wateja watarajiwa kupitia tovuti yake (lead generation)
  7. Kuhakikisha ana wafuasi kwenye mitandao ya kijamii (Social Media Marketing)

Na listi ni ndefu.

Hizo zote ni bidhaa ambazo mtu anayetengeneza tovuti anaweza akauzi juu ya huduma yake ya kutengeneza tovuti.

Japokuwa sishauri afanye yote, lakini akijikiti kwenye mawili au matatu ya ziada basi kipato kitaongezeka maradufu.

Jinsi Ya Kutumia Mtandao Kunasa Wateja Kama Smakuhttps://onlineprofits.co.tz/mtandao

Njia ya Uhakika Ya Kupata Kipato Endelevu

Mwandishi wa kitabu cha Rich Dad Poor Dad, katika kitabu kiitwacho Who Took My MoneyRobert Kiyosaki anasema,

There are 2 types of business owners. The cattle ranchers and the dairy farmers.

One of the reasons so many people lose so much money is because they invest like ranchers.

They invest to slaughter rather than to milk.

Yaani…

Kuna aina mbili ya wafanyabiashara. Wanaomiliki ng’ombe kuuza nyama na wanaomiliki ng’ombe kuuza maziwa. Sababu kubwa wafanyabiashara wengi wanapoteza pesa ni kwa sababu wanafanya biashara kama wanaomiliki ng’ombe wa nyama.
Wanawekeza kuuza nyamba badala ya kuuza maziwa. 

Kwa lugha rahisi, anayemiliki ngombe wa kuchinja atauza mara moja, na anayemiliki ng’ombe wa mazima atauza mazima kwa miaka kumi au zaidi kwa ng’ombe yule yule.

Kwa hivyo katika biashara yako unatakiwa kuwa na ng’ombe mwenye kutoa maziwa ili uwe unapata kipato mara kwa mara.

Unatakiwa kuwa na huduma ambayo itamfanya mteja awe anakuja kwako mara kwa mara jambo ambalo litafanya biashara yako inakuingizia pesa hata kama hupati wateja wapya.

Kwa hivyo jiulizwe swali, kitu gani naweza kufanya kwenye biashara yangu itakayosababisha wateja kuja kwangu mara kwa mara?

Kama unafanya biashara ya kutengeneza tovuti, unaweza ukatoa huduma ya ukarabati wa kudumu wa tovuti na mteja wako akawa anakulipa kwa mwezi au kwa mwaka.

Kama unauza bidhaa kama nguo, vipodozi au viatu jiulize wateja wangu huwa wananunua vitu kama hivi kila baada ya muda gani?

Kama wengi wao wananunua kila baada ya miezi mitatu basi inabidi uweke mfumo ambao utashusha mizigo mipya kila baada miezi mitatu na kuwafanya wao waje kwako wakati huo.

Unaweza ukaanzisha VIP club kwa wateja wako wanaonunu mara kwa mara na mzigo ukifika tu unawakaribisha waje dukani kwako wachague kabla hujaanza kuziweka hadharani.

Kama bidhaa zako ni za kiwango cha juu ambazo ni nadra kupatikana nakuhakikishia ng’ombe wako atakulea maziwa mpaka uchoke wewe.

Kama mfumo wako utakuwa unarudisha idadi ya wateja wako 100 kila mwezi basi utakuwa umezidisha kipato chako mara 2 kila mwezi bila ya kuongeza wateja wapya.

Hii ndiyo formula ya uhakika ya kuongeza kipata kwenye biashara yako bila ya kuongeza wateja. Kujifunza zaidi, angalia video ya “Njia Tatu Pekee Za Kukuza biashara hapa Chini

Je wewe unatumia njia zipi kati ya hizi?

Nijulishe kwa kuandika maoni yako hapo chini bila ya kusahau kusambaza Facebook na Whatsapp kwa kubofya kitufe husika hapo chini.

Wako mwenye kupenda maendeleo yako,

Dr. Said Said 


Ujumbe Wa Facebook

    5 replies to "Jinsi Ya Kuongeza Kipato Kutoka Kwa Wateja Wachache"

Leave a Reply

Your email address will not be published.