Kama wewe ni mjasiriamali unayehangaika kupata wateja kupitia matangazo yako basi formula hii ya AIDA itakupa mafanikio makubwa katika matangazo yako kuliko formula nyengine yoyote.

Lakini kabla ya kuangalia fomula hiyo kwanza ningependa niongelee aina za matangazo.

Kuna aina mbili kubwa za matangazo

1: Institutional Advertising:

Aina hii ya matangazo ni matangazo yanayozungumzia kampuni/biashara yako, bidhaa au huduma unayotoa.

Kwa jina jengine tunaweza kuiita branded advertising au ‘ME Advertising‘ yaani tangazo lako lina focus kuisifia kampuni au bidhaa unayouza.

Na tunaweza kuona matangazo ya aina hii kwenye TV, Radio na magazeti.

Mifano mizuri ni matangazo ya Tigo, CocaCola na brand nyingi kubwa kubwa.

Hakuna ubaya katika aina hii ya matangazo isipokuwa matangazo haya yanahitaji uwe na subira katika kupata matunda.

Yaani unatakiwa uwekeze kwa kiasi kikubwa mpaka watu waone matangazo yako sana hadi kuja kuizoea na kuiamini kabla ya kuanza kununua bidhaa na huduma unayotoa.

Kama biashara yako ni ndogo na sio kubwa kama Tigo, Airtel au vodacom basi Institutaional Advertising inaweza ikakutia hasara na kuiua biashara yako.

Kwa hivyo kama wewe ni mjasiriamali mdogo au wa kati na unataka kuona faida mara moja baada ya kufanya matangazo, njia nzuri unayoweza kutumia kutangaza biashara yako ni kufanya…

2: Direct Response Advertising.

Hii ni aina ya tangazo ambayo badala ya kujizungumzia au kujisifu wewe (Me Advertising), focus yako inakuwa kuzungumzia shida na utatuzi wa matatizo ya mteja wako; ‘YOU Advertising’.

Angalia mfano ufuatao ili uweze kuelewa kwa undani tofauti kati ya institutional advertising na direct response advertising.

Chukulia mfano ninamiliki hospitali; “Dr. Said’s Clinic“.

Kama nitaamua kutangaza hospital yangu kupitia institutional advertising, tangazo langu litakuwa kama lifuatayo,

Dr. Said’s Clinic ni kliniki bora kuliko zote za Dar.

Vifaa na vipimo vyake ni vya kisasa kabisa na madaktari wake wamebobea katika fani zao.

Karibu sana Dr. Said’s Clinic Upate huduma bora za afya.

Katika tangazo hili sio rahisi msikilizaji kukuamini 100% kwa sababu

  1. Hakujui, hakupendi na wala hakuamini
  2. Kila mwenye kufanya tangazo kama hilo anajisifu kuwa yeye ndio bora kuliko mwenzake.

Kwa hiyo kwa kuweka tangazo hilo sio rahisi kuwashawishi watu wa kutosha kuja kupata huduma katika hospitali yako japokuwa wapo baadhi ya watu wanaweza kufika kutokana na tangazo hili.

Ila nikifanya tangazo hili kwa kutengeneza tangazo la Direct Response Advertising tangazo litakuwa kama hivi…

“Ujumbe Muhimu Sana Kwa Wagonjwa Wa Sukari

Kama wewe ni mgonjwa wa sukari ambaye umekuwa unahangaika kwa muda mrefu na tatizo hilo bila ya kupata utatuzi wa uhakika basi naomba unisikilize kwa makini kabisa kwani huenda taarifa ifuatayo ikawa taarifa muhimu kuliko taarifa yoyote katika maisha yako.

Baada ya kuwasaidia zaidia ya wagonjwa 845 wa sukari nimekuja kugundua kuwa chanzo cha tatizo la ugonjwa huo sio kula vyakula vya uwanga kama madaktari wengi wanavyodai bali ni jambo ambalo ukilifahamu utaweza kuondokana na tatizo hilo mara moja bila ya kumeza dawa kila siku.

Ndani ya taarifa hii fupi nitazungumzia chanzo cha tatizo lako na mambo 5 ya kuzingatia kuweza kutatua tatizo hilo na jambo gani la kufanya mara moja kuweza kutokomeza tatizo hilo sugu…

… Milele.”

Kwa hiyo hapo sijaizungumzia hospitali, sijajizungumzia mimi na wala sijazungumzia product au huduma ninazotoa.

Bali nimezungumzia tatizo la mteja na suluhisho lake.

Kwa hiyo ndani ya makala hiyo ninazungumzia tatizo la mteja na suluhisho lake.

Na mwisho kabisa ninaweza kumalizia tangazo kwa style hii…

Kama umefaidika na taarifa hii na utapenda kuonana na mimi ana kwa ana kwa ajili ya ushauri wa BURE KABISA kupata muongozo wa kutatua tatizo lako piga simu namba 0719 XXX-XXX.

Ofa hii ya kupata ushauri wa BURE ni kwa watu 10 tu. Hao watu 10 wakiisha, ushauri huo utakugharimu Tshs. 65,000.

Ili usipitwe na hiyo OFA hakikisha unafanya booking sasa hivi kwa kupiga simu 0719 XXX-XXX. Atapokea msaidizi wangu Ghalya Said. Mwambie kuwa unataka kuweka booking kwa ajili ya kupata ushauri wa BURE na yeye atakujuza muda gani nitakuwepo FREE kwa ajili yako.

Kama simu haipatikani jaribu tena. Na tena. Na tena.”

Kwa hiyo hapo mgonjwa yeyote wa sukari akishasoma hiyo makala kuna uwezekano mkubwa wa kupiga simu na kuweka booking.

Kwa vile focus yangu ilikuwa ni mteja na sio clinic yangu, haijalishi ushauri wangu nitaufanya wapi.

Nishamuonyesha mteja kuwa ninafahamu matatizo yake na nina suluhisho ya matatizo hayo.

Kwa hiyo tofauti kubwa iliyopo kati ya Institutional Advertising na Direct Response Advertising ni kwamba Institutional Advertising ina focus kwenye kampuni  au huduma unazotoa (ME Advertising) wakati Direct Response Advertising ina focus kwa wateja (You Advertising).

Njia nzuri na ya haraka kunasa wateja kupitia tangazo lako ni ya kufocus kwa wateja.

Jinsi ya Kutumia Formula Ya Aida Kwenye Matangazo Yako

AIDA formula.

A: Attention Grabbing Headline

Hiki ni kichwa cha habari chenye mvuto.

Kwa hiyo kama una bidhaa inayosaidia watu kupunguza uzito, unaweza ukaandika kichwa cha habari kama ifuatavyo:

“Jinsi ya Kupunguza Kilo 5 Ndani Ya Siku 5 Bila ya Kufanya Mazoezi Au Kumeza Dawa”

Kichwa cha habari kizuri ni kile kinachoelezea jinsi ya kusolve tatizo.

Kujifunza zaidi kuhusiana na Jinsi ya Kuandika Vichwa Vya Habari Vyenye Mvuto, angalia video hii:

I: Interest

Unatakiwa kumfanya mtu aendelee kusoma tangazo, lengo la Kichwa cha habari ni kumfanya mtu asome mstari wa kwanza wa Tangazo na lengo la mstari wa kwanza ni kumfanya mtu aendelee kusoma mstari wa pili hivyo hivyo hadi mwisho wa tangazo.

Mfano wa Interest ni kama maneno yafuatayo:

“Kama wewe ni mgonjwa wa sukari ambaye umekuwa unahangaika kwa muda mrefu na tatizo hilo bila ya kupata utatuzi wa uhakika basi naomba unisikilize kwa makini kabisa kwani huenda taarifa ifuatayo ikawa taarifa muhimu kuliko taarifa yoyote katika maisha yako.”

Kama unavyoona, sentensi hiyo inamfanya msomaji atake kusoma zaidi kujua kuna taarifa gani mbele. Kwenye elimu ya saikolojia inaitwa ‘Open loop’ yaani msomaji anaambia atapewa kitu fulani na ili akipate aendelee kusoma.

Wanaotengeneza tamthilia wanaifahamu sana hii saikolojia. Story inaishia kati kati na wewe unabakishwa na hamu ya kutaka kufahamu mwisho wake itakuwaje.

D: Desire

Unataka msomaje awe na hamu ya kuchukua hatua.

Kufanya hivyo inabidi utoe OFA ya kufa mtu kiasi ambacho kitamfanya ajione mpumbavu kama hajachukua hiyo OFA.

Hiyo ndio inasabibisha damu yake mwilini kuwaka moto na kutaka kuchukua hatua haraka.

Vitu vitakavyomhasisha kuwa na hamu kuchukua hatua ni

  1. Unatoa kitu cha thamani BURE kabisa (kama ushauri wa bure)
  2. Unatoa OFA kwa muda mchache (mwisho wa OFA ni kesho saa nane mchana)
  3. Unatoa ushuhuda wa watu wenye matatizo kama yao kuweza kupata suluhisho la tatizo lao kupitia bidhaa/huduma yako.
  4. Unatoa 100% Money Back Guarantee.

A: Action

Hapa unamwelekeza msomaji (mtazamaji/msikilizaji) kufanya nini exactly kupata anachotaka kupata.

Kwa mfano katika tangazo unamwambia,

“Kufanya booking Piga simu namba 0719 XXX-XXX. Atapokea msaidizi wangu Ghalya Said. Mwambie kuwa unataka kuweka booking kwa ajili ya kupata ushauri wa BURE na yeye atakujuza muda gani nitakuwepo FREE kwa ajili yako. Kama simu haipatikani jaribu tena. Na tena. Na tena.”

Inashauri zaidi kutotangaza bidhaa kwenye Direct Response Advertising isipokuwa kama unatangaza kwa watu wanaokujua, kukupenda na kukuamini.

Kwa wateja wapya toa kitu bure uanze kujenga uaminifu kwao kabla ya kuuza bidhaa au huduma.

Unataka kuona mfano halisia wa Direct Response Advertising?

Angalia video ifuatayo:

Nakuhakikishia kama utaanza kutumia fomula hii katika matangazo yako, utaanza kuona matunda yake baada ya muda mfupi.

Je umependezeshwa na makala hii?

Utachukua hatua na kuandaa tangazo la Direct Response Advertising?

Kama jibu ndio, comment chini na share hii makala Facebook kwa kubofya kitufe cha ‘share’ chini.


Ujumbe Wa Facebook

Leave a Reply

Your email address will not be published.