Woga ni kitu ambacho watu wote wanacho, hakuna mtu anayeishi duniani na ikawa hakuna kitu

asichokiogopa na kama yupo mtu wa aina hiyo basi atakuwa ana matatizo ya akili. Lakini kwa wenye akili,

kila binadamu duniani lazima atakuwa ana kitu kinachomfanya awe na woga fulani.

Wengi wetu huwa tunafikiria kuwa woga ni kitu kibaya, lakini ukweli ni kwamba woga si kitu kibaya, kwa

kweli woga ni kitu kizuri na ni ishara ya  kuwa unatakiwa kuchukua tahadhari au kujiandaa na hilo jambo

linalokutia uwoga. Kwa mfano kama huna kazi na umeishiwa na pesa na unatakiwa ulipie pesa ya chumba

unachoishi uwoga unakuja. Hivyo unatakiwa ujiandae kwa kwenda nje kupambana na kutengeneza pesa

ambayo itakuwezesha kulipa kodi ya chumba unachoishi. Huo ndio uwoga.

 

Lakini cha ajabu na tofauti ya watu wanaofanikiwa na watu wanaohangaika katika kupata mafanikio ni

kwamba watu wenye mafanikio huwa wanajua kwamba kitu ambacho naogopa kufanya ndio natakiwa

kukifanya ili kupata mafanikio. Na wale ambao hawafanikiwi huwa wanakimbia ule woga wao, yaani hawapo

tayari kufanya kile wanachokiogopa. Kwa kiingereza uwoga unajulikana kama FEAR, herufi hizi zina maana

ya kwamba false evidence appear real, ikiwa na maana vitu vya uongo au ushahidi wa uongo

unaoonekana kama kweli.

 

Kwa hivyo ukiogopa kitu huwa unatengeneza picha ambayo si ya kweli. Kwa mfano kama unaogopa kuanza

biashara unaweza kutengeneza picha ya kwamba nikifanya hivi watu watanicheka, au pesa yangu itazama au

nitashindwa kuiendesha, vitu ambavyo havina ukweli wowote ndani yake. Watu wa saikolojia wanasema

“Woga unawaumiza sana watu kuliko kufeli” yaani ni bora ukafanya kitu unachohofia kisha ukafeli kuliko

kuwa hujafanya kabisa kwa sababu ya uwoga wako. Hii ni kwa sababu ukifanya kitu hata kama ukafeli lakini

tayari kuna mambo utakuwa umejifunza na wakati ujao unaweza kuyakwepa yale yaliyokufelisha mara ya

kwanza.

 

Hivyo kama una jambo ambalo sasa hivi unatakiwa ulifanye lakini haulifanyi kwa sababu unaogopa.

Nakuhakikishia kama utafanya maamuzi na kuanza kulifanya hilo jambo  linaweza kukutoa katika matatizo

uliyokuwa nayo sasa hivi.

 

Watu wengi huwa wanapenda kuniuliza Dr. said nifanye nini ili nipate mafanikio, au ni nini siri ya mafanikio?.

HAKUNA SIRI YA MAFANIKIO, Mafanikio ni kufanya tu yale mambo ambayo unatakiwa kufanya lakini

unatafuta kila sababu ya kutofanya.

 

Mfano mzuri hivi karibuni nilitoa challenge kupitia Group la WhatsApp la Online Profits, kwamba kila mtu

arekodi video moja inayoelezea biashara yake. Challenge hii niliitoa kwa watu zaidi ya mia tatu (300) lakini,

ni mtu mmoja tu ndiye aliyenitumia video aliyorekodi. Baada ya hapo watu wanakuja tena na kuuliza Dr.

Said nifanye nini ili nipate mafanikio, jibu ni kwamba fanya kile unachoogopa kufanya utafanikiwa. Kama

sasa hivi kuna kitu unaogopa kukifanya anza nacho hicho kila siku.

 

Nakupa challenge kwamba kila siku ukiamka andika vitu ambavyo unatakiwa uvifanye, kisha angalia ni kipi

unakiogopa kati ya hivyo na uanze na hicho. Nakuhakikishia hicho kimoja unachokiogopa ukikifanya

kitakupa mafanikio makubwa kuliko vingine.

 

Je, wewe ni mfanyabiashara na unahangaika kupata wateja? Kama jibu ni ndio, basi habari njema kwako ni

kwamba tumekuandalia kozi ya “Jinsi ya Kutumia Facebook na Instagram Kunasa Wateja.” Kuanza

Kusoma Kozi Hiyo Bonyeza Hapa.

 

Kama una swali unaweza kuliacha kupitia comments hapo na usisahau kuwashirikisha wengine kwa

kubonyeza vitufe vya mitandao ya kijamii hapo chini.


Abdallah Hemedi
Abdallah Hemedi

Content Manager

Ujumbe Wa Facebook

Leave a Reply

Your email address will not be published.