Kama wewe una bidhaa au huduma unayotoa na unataka kujua njia rahisi ya kutumia kupata wateja kupitia mtandao basi hakikisha unasoma makala hii mpaka mwisho.
Ndani ya aya zijazo utajifunza njia moja rahisi na ya uhakika unayouweza kutumia kupata wateja kupitia mtandao.
Na njia hii ni bora kuliko;
- kutangazia bidhaa au huduma unazotoa
- Kuwa na followers wengi Facebook au
- Kuwa na followers wengi Instagram
Japokuwa ukitumia njii hii huku una followers wengi katika mitandao ya kijamii, itasakusaidia sana kuuza bidhaa na huduma unazotoa.
Nji yenyewe ni….
Kuelimisha na kuwapa taarifa wateja wako watarajiwa.
Kwa kiingereza inaitwa ‘educational based marketing‘ ambayo inasifika kuwa ndio moja ya aina ya njia masoko yenye tija kuliko njia nyenginezo.
Kwa nini uwaelimishe wateja wako watarajiwa?
Badala ya kuongelea jinsi gani kampuni yako, bidhaa au huduma unazotoa ni nzuri, waelimishe namna ya kutatua matatizo yanayowasibu.
Na ukifanya hivyo utauza sana kuliko kutangaza bidhaa au huduma unazotoa kwani utakuwa unajiweka kwenye soko kama mtaalamu (expert) na sio muuzaji/mfanyabiashara.
Huniamini?
Hebu angalia jedwali ifuatayo;
Asilimia kubwa ya watumiaji wa mtandao wa intaneti wanatumia tovuti kama Google kutafuta taarifa za vitu vyenye kuwaelimisha au matukio fulani (Informational search).
Kama ana chunusi ataenda Google na kuchapa ‘jinsi ya kuondoa chunusi haraka‘.
Kama ni mnene na anataka kupunguza uzito atachapa ‘jinsi gani ya kupunguza uzito haraka bila ya kufanya mazoezi‘
Ni wachache sana (kama unavyoona kwenye jedwali hapo juu) watachapa ‘dawa ya kuondoa chunusi‘ au ‘dawa ya kupunguza uzito.‘
Hatua za kufuata za kuwaelimisha wateja wako watarajiwa:
- Jua wateja wako watarajiwa wanasumbuliwa na nini. Waulize ikiwezekana. Nenda katika ma forum kama Jamii Forums uone maswali wanayouliza.
- Tumia blog (kama hii) kuwaelimisha wateja wako watarajiwa kwa mfumo wa maandishi na hata video.
- Toa OFA zako mwisho wa kila makala yako
- Pokea wateja
Natumai umefaidika na makala hii.
Hii hapa ni OFA yangu kwako:
Kama huna blog na unataka kutengenezewa blogu bure basi wasiliana nasi hapa.
(NB: Utahitaji kulipia usajili wa domain yako (jina-la-blog-yako.com) na urushaji wa blogu yako (hosting))
Naomba unisaidie kusambaza Facebook na WhatsApp kwa kubofya vitufe husika hapo chini ili na wengine wapate faida.
Na vile vile naomba uniambie kwa ku comment hapo chini;
Unakumbana na changamoto gani katika kujenga biashara yako mtandaoni?
Nitajitahidi kukujibu na kukupa ushauri.
Hadi hapo siku nyengine,
Ni mimi mwenye kupenda mafanikio yako,
Dr. Said Said