Moja ya maswali ninayoulizwa mara kwa mara kutoka kwa wajasiriamali hususan wanaojaribu kupata wateja kupitia mtandao ni “kwanini watu hawanunui kutoka kwangu“?

Jambo hili linawaumiza kichwa sana mpaka wengi wao kukata tamaa kabisa.

Kama na wewe ni mjasiriamali na unashindwa kutumia mtandao kuuza bidhaa au kupata wateja basi naomba unisikilize kwa makini kwani jibu la swali hili litakufanya uwe na mtazamo tofauti wa biashara kwa ujumla na kufuata mbinu yenye kukuletea wateja kwako kama smaku mbinu ambayo ni kinyume na unayotumia hivi sasa kupata wateja.

Wajasiriamali wengi wanadhania kuwa bidhaa zenye kuuza sana kwenye mtandao ni zile zenye ubora (high quality).

Japokuwa bidhaa zenye ubora huuza zaidi, hiyo sio sababu ya msingi inayowafanya wateja wasinunua kutoka kwako.

Sababu ya msingi inayowafanya wateja wasinunua kutoka kwako ni …

IMANI

Sio bidhaa yako, sio huduma yako, sio kampuni au ofisi yako.

Ni kutoamini.

Aidha

  1. Hakuamini wewe
  2. Haamini kuwa bidhaa au huduma unazotoa itatatua matatizo yake
  3. Hajiamini yeye mwenyewe

1: Hakuamini Wewe

Asilimia kubwa ya wateja wako watarajiwa hawakuamini na ndio maana hawanununi kutoka kwako.

Kwa nini hawakuamini?

Kwa sababu anaona kuwe lengo lako kuu ni moja…..

Kuuza bidhaa na kutengeneze pesa.

Haamini kuwa upo pale kumsaidia kutatua matatizo yake.

Na kusema la ukweli, mara nyingi yupo sahihi.

Unajua wafanyabiashara wengi tuna tatizo moja kubwa.

Tunawaza sana kutengeneza pesa! 

Akili zetu zimezungukwa katika kuuza bidhaa au huduma ili tutengeneze pesa haraka.

Japokuwa hakuna ubaya kuwaza kutengeneza pesa lakini jambo la muhimu kufahamu ni kuwa…..

Lengo la biashara sio kutengeneza pesa.

Lengo la biashara ni kutatua matatizo ya wateja wako watarajiwa.

kutengeneza pesa ni matokeo ya lengo lako.

Kwa hivyo kama hujatatua au hujamuonyesha mteja wako kuwa una nia safi ya kutatua tatizo lake, huna haki ya kutengeneza pesa, kwani lengo litakuwa halijafikiwa.

Jinsi ya kujenga uaminifu kwa mteja wako mtarajiwa

Kwa vile ushajua lengo lako ni kutatua matatizo ya wateja wako watarajiwa, kinachofuata sasa ni kuhakikisha unawapa suluhisho ya matatizo yao kabla ya kuwauzia chochote.

Mtaalamu mmoja wa mambo ya masoko ya mtandao (Internet Marketer) kwa jina la Perry Marshall ana msemo wake unaosema:

Anybody who bought a drill NEVER wanted to buy a drill. They wanted to make holes.

if you want to sell drills DO NOT advertise the drill. Advertise ‘how to make a hole.’

Yaani,

Kila mwenye kununua drili hakutaka kununua drili. Alitaka kutoboa ukuta.

Kwa hivyo ukitaka kuuza drili, usitangaze drili. Tangaza ‘Jinsi ya kutoboa ukuta’.

Kwa hivyo badala ya kutangaza tu bidhaa kwa watu wasiyokufahamu, jiulize kwanza hawa watu wana matatizo gani? Ikisha tangaza utatuzi wa matatizo ya wateja wako.

Kwa mfano kama una bidhaa yenye kuwasaidia wateja wako watarajiwa kupunguza uzito unaweza ukaandika makala kama hii niliyoandika mimi, ukatengeneza video au ukatoa ushauri wa bure yenye kuwafahamisha (k.m)…

“Njia 5 za Kupunguza Kilo 10 Ndani ya Wiki Moja Bila Ya Kufanya Mazoezi”  

Kufanya hivyo utakuwa umetimiza malengo yafuatayo:

  1. Umemuelimisha mteja wako mtarajiwa.
  2. Umemuonyesha namna ya kutatua tatizo lake bila ya kudai pesa.
  3. Umejenga uaminifu kwake na
  4. Umejiweka kwenye soko kama mtaalamu wa kuwasaidia watu kupunguza uzito jambo ambalo litakufanya uaminike kwenye soko na kukutofautisha kwa kiasi kikubwa na washindani wako.

Mwisho wa makala/video yako unaweza kusema japokuwa zipo bidhaa tofauti zenye kusaidia kupunguza uzito kwa kiasi kikubwa, bidhaa hii (taja jina la bidhaa) imeonekana inafanya hivyo kwa usalama na kwa gharama ndogo kulinganisha na bidhaa nyengine.

Kupata sampo ya bidhaa hii piga simu namba …… (toa namba yako ya simu).

NB: Tafadhali kuwa mkweli. Kama hujathibitisha kuwa bidhaa/huduma yako inaweza kutatua tatizo la mteja wako mtarajiwa tafuta bidhaa au toa huduma yenye kutatua matatizo ya walengwa wako hata kama itakuwa ni bei ya juu. Kumbuka kuwa lengo lako sio kuuza bidhaa bali kutatua matatizo ya wateja wako. 

2: Hawaamini Bidhaa Zako

Japokuwa mara nyingi mteja mwenye kukuamini hununua bidhaa yako, wapo ambao hawatofanya hivyo.

Na sababu kubwa ni kuwa anawasiwasi bidhaa au huduma ile japokuwa imewasaidia wengine, haitosaidia yeye binafsi.

Mimi binafsi nilipata tabu sana kuuza huduma zangu japokuwa nilijenga uaminifu baada ya kuwashauri na kupenda sana ushauri wangu.

Cha kushangaza baadhi yao waliogopa kufuata ushauri wangu wakiamini kuwa ushauri wangu wa kisomi na hauendani na mazingiria yetu ya kitanzania.

Waliniamini lakini hawakuamini kuwa bidhaa/huduma ninayotaka kumpa kuwa itamfaa yeye.

Jinsi Ya Kuwafanya Waamini Bidhaa Zako

Kuna njia kubwa 2 kubwa ya kuwafanya wateja wako watarajiwa wakuamini (njia ambazo mimi binafsi nilitumia).

  1. Toa Guarantee ya bidhaa / huduma zako: Unamwambia mteja yafuatayo.”Sikiliza! Najua una wasi wasi bidhaa / huduma hii haitokusaidia. Ili kukuondolea wasi wasi huo, nakupa guarantee ya kutumia bidhaa hiyo kwa siku 60 zijazo. Kama hukupata mafanikio/maendeleo kutaokana na bidhaa hiyo, nirudishie na mimi nitakurudishie 100% ya pesa zako bila ya kukuhoji chochote.”Na guarantee yako yaweke kwa maandishi ili awe na amani ya kununua kutoka kwako. Kama bidhaa yako ni nzuri kweli (na unatakiwa kuwa na bidhaa/huduma nzuri) hutakiwi kugopa kutoa guarantee. 
  2. Toa bidhaa au huduma BURE! Badala ya kujaribu kumshawishi mteja wako kuamini bidhaa yako itamsaidia, mpe sampo ya bidhaa au huduma BURE kabisa. Akishaona faida atakuja kwako kununua. Ukifanya hivyo ataona kuwa kweli una nia safi ya kumsaidia kutatua matatizo yao na hupo pale kutengeneza pesa tu.

3: Hajiamini Yeye Mwenyewe

Kama bidhaa au huduma yako unayotoa inahitaji mteja wako afanye kazi kwa namna moja au nyengine basi baadhi yao hawatonunua bidhaa hiyo kwa kuhofu watashindwa kufanya kazi.

Kwa mfano kama unatoa huduma ya mazoezi inayomhitaji yeye kuja kwenye gym yako mara kwa mara hali ya kuwa anajijua kuwa yeye ni mvivu, basi anaweza kukataa kununua kutoka kwako japokuwa anakuamini na OFA yako ni nzuri.

Jinsi Ya Kumpa Imani Mteja Wako Mtarajiwa:

Ili kuondoa tatizo hili ni muhimu mteja aone:

  1. Hatua anazotakiwa kufuata kutatua matatizo yake ni chache na rahisi: Kwa mfano umuonyesha kuwa kuna hatua 3 za kufuata kufikia malengo anayotaka kufika na pengine anahitajia kutumia masaa 3 kwa wiki.
  2. Wapo watu kama yeye waliyoweza kupata mafanikio na huduma yako: Hapa unamuonyesha kuwa wapo watu wenye hali kama yake au mbaya kuliko yake na wakafuata hatua hizo na kufanikiwa. Kwa hivyo kumuonyesha ushuhuda ya wateja wengine itamuondolea uzito wa yeye kutonunua bidhaa / huduma kutoka kwako.

Kinachofuata ni nini?

Ukifanya yafuatayo utaanza kupata wateja wengi kwenye biashara yako na biashara yako itakuwa kwa kasi kubwa:

  1. Hakikisha unaelewa matatizo ya wateja wako watarajiwa. Ongea nao. Waulize wakwambie.
  2. Hakikisha una bidhaa / huduma nzuri yenye kutatua matatizo yao. Kama bidhaa/huduma zako ni ya ubora wa chini, basi hakikisha unatafuta bidhaa yenye sifa nzuri za kutatua matatizo ya wateja wako japokuwa ni ghali kuliko bidhaa ulozinazo sasa hivi.
  3. Tangaza utatuzi wa matatizo ya wateja wako, usitangaze bidhaa huduma zako.
  4. Wachukulie wateja wako kama ndugu na marafiki zako wanaokuamini kuwa una nia moyo safi kwao na upo tayari kufanya chochote kuwasaidia kutatua matatizo yao.

Ukishaweza kufanya hayo hakuna mshindani atakayekusumbua kichwa.

Kama umependa makala hii basi utapenda zaidi kujiunga kwenye group letu la WhatsApp.

BOFYA HAPA kujiunga

Ndani ya group hii utapata kujifunza mbinu tofauti za kutumia kwenye mtandao kunasa wateja kama smaku.

Mafunzo hayo yanatolewa kwa njia ya maandishi, audio na video na tunajibu maswali yoyote wanagroup watakayokuwa nayo.

Japokuwa wanachama wa group huliipa ada ya shs. 20,000/- kwa mwezi tunakupa OFA ya mwezi wa kwanza BURE ujionee kabla hujaji commit kulipa.

Kama hujaridhika na mafunzo hayo ndani ya huo mwezi unaruhusiwa kutoka bila ya kulipa gharama yoyote.

Kama utapenda kujiunga BOFYA HAPA tukuingize mara moja kabla ya group kujaa.

Je wewe unahisi sababu kubwa watu hawanunui kutoka kwako ni nini?

Comment hapo chini.

Na naomba utusaidie kusambaza makala hii katika mitandao ya Facebook, WhatsApp na mengineo kwa kubofya vitufe husika ili na wengine wafaidike.

Hadi hapo makala mengine,

Ni mimi Dr. Said Said,

Mwenye kujali mafanikio yako


Ujumbe Wa Facebook

Leave a Reply

Your email address will not be published.