Enzi za miaka ya 85 hadi 95 yalikuwa na raha sana kwa wafanyabiashara hapa Tanzania…..

Nchi ilikuwa inatoka katika siasa za ujamaa na kujitegema na kufuata mfumo mpya uliowapa watu ruhsa‘ ya kushiriki katika biashara kwa uhuru zaidi.

Wafanyabiashara hao waliruhusiwa kuagiza bidhaa tofauti kutoka nje kwa ajili ya kukidhi haja za wananchi ikiwemo vyakula, vifaa vya ujenzi, nguo n.k.

Na wananchi nao walikuwa tayari kupokea vitu hivyo kwani nchi ilikuwa katika uhaba wa hivyo vitu.

Matangazo ya biashara wakati huo yalikuwa yakisomwa na kusikilizwa kwa hamu kwani matangazo hayo yaliwapa watu matumaini ya mabadiliko kwenye maisha yao na kuwafunua macho katika dunia mpya ya utandawazi.

Kwa ufupi, WAFANYABIASHARA WALIKUWA NI WAFALME!

Walikuwa wachache, mahitaji yalikuwa ni mengi na matangazo yoyote waliokuwa wakiyatoa yalikuwa yakisikilizwa na kuleta tija kubwa kwenye biashara zao.

Na televisheni ilivyoanza kuenea majumbani mwa watu, mafanikio yao yaliendelea kuzidi.

Mambo yalivyoanza kuwa Magumu

Ushindani ulivyozidi kuwa mkubwa, na matangazo kuwa mengi, wafanyabiashara wengine walianza kupoteza soko katika biashara zao.

Na wale waliyoongeza ubunifu japo kidogo kwenye matangazo ndio waliyoendelea kutawala katika kupata wateja katika biashara yao…..

…..lakini sio kwa muda mrefu.

Mabadiliko Katika Ulimwengu Wa Intaneti na Mitandao Ya Kijamii

Ulimwengu wa intaneti na mitandao ya kijamii ilivyoingia nchini, watumiaji wameanza kuwa na sauti mbele ya umma.

Ulimwengu wa zamani ambao mfanyabiashara anaweka tangazo na kusikilizwa (japokuwa bidhaa na huduma zake ni mbaya), umeanza kufifia. Wasikilizaji na watazamaji wa matangazo hayo wamekuwa na uwezo mkubwa wa kukusema vibaya hadharani na kuvuruga heshima ya biashara yako.

Kwa ufupi, MTEJA AMEKUWA MFALME MPYA

Na nikisema mfalme namaanisha kuwa mteja amekuwa na nguvu kama ya mfanyabiashara (kama sio zaidi) katika kutengeneza au kuharibu biashara yake.

Tukiangalia nchi za magharibi zipo mifano mingi ambayo mteja alihudumiwa vibaya na baada ya mteja yule kuelezea yaliyomsibu katika mitandao ya jamii, imepelekea kampuni husika aidha kumfukuza mfanyakazi, kuomba msamaha hadharani au mpaka kampuni kufa.

Na tunaona mwenendo huu huu ukijitokeza katika mitandao yetu ya kijamii ya hapa kwetu.

Huu hapa ni mfano mmoja:

banc ABC Matapeli Jamii Forums

ABC Matapeli - jamii Forums

[NB: Mfano nilioutumia hapo juu ni kwa lengo la kuelimisha tu na sio kwa kuwasema vibaya Banc ABC. Mimi binafsi ni mwanachama wa Banc ABC na hawakuwahi kunifanyia jambo lenye kunikera.]

Kama uonavyo hapo juu, huyo mteja hakufurahishwa na vitendo alivyofanyiwa na benki hiyo na ametumia ufalme alionao kuweka malalimiko yake kwa kuanzisha nyuzi katika mtandao wa kijamii wa Jamii Forums kitu ambacho kimesababisha wanachama mbali mbali wa mtandao huo kuchangia, wengi wao kwa kuwasema vibaya. 

Solution Kwa Wafanyabiashara

Sio siri kuwa kila siku zinavyokwenda, sauti ya wateja inakuwa kubwa kuliko sauti ya wafanyabiashara.

Kwa hivyo kama wewe ni mfanyabiashara unayetaka mafanikio katika ulimwengu huu wa mitandao ya kijamii, unatakiwa kubadilisha mbinu za kuendesha na kutangaza biasharaka yako kwa ‘digirii 180‘.

Usipofanya hivyo usalama wa biashara yako itakuwa hatarini na wateja wako watakuchukia na kusambaza chuki zao katika mitandao tofauti.

Ila kama unataka uwe unasikilizwa, upendwe na upate wanunuzi wengi wa bidhaa na huduma zako kushinda wapinzani wako basi huna budi isipokuwa kufanya yafuatayo:

    1. Kuwa na Nia Safi Ya Kutoa Huduma Kwa Wateja Wako

     Kuwa Na Nia SafiEnzi za kuuza na bidhaa na huduma kwa lengo la kutengeneza pesa imepitwa na wakati. Na ukiendelea kufanya hivyo hutodumu kwa muda mrefu kabla ya kugaragazwa na wateja wako.

     Fuata ushauri wa Brian Tracy aliposema,

     Making money is not the Goal of your business. Making money is the outcome. The goal of your business is attaining customer satisfaction by solving his/her problems.

     Yaani:

     Kutengeneza pesa sio lengo lo biashara yako. Kutengeneza pesa ni matokeo. Lengo la biashara yako ni kumfurahisha mteja baada ya kutatua matatizo yake.

    2. Tengeneza Jukwaa Kwenye Mtandao Lenye Kukaribisha Mazungumzo Kati Yako Na Wateja Wako (na Wateja Watarajiwa):

     Jukwaa

     Kwa vile mteja wako ndio mfalme, huna budi isipokuwa kumsikiliza ili kuelewa mahitaji yake na kumuonyesha njia ya kutatua matatizo yake.

     Na hakuna jukwaa zuri la kuzungumza na wateja wako (na unaowatarajia) kwenye biashara yako kama blogu.

     Blogu inakupa fursa za kuzungumza na maelfu ya wateja wako (na watarajiwa) kupitia makala zako (kama hii unayoisoma hapa).

     Blogu inawapa elimu na maarifa wasomaji wako, jambo ambalo linaleta ukaribu, uaminifu na kuwaandaa kisaikologia kuwa tayari kununua bidhaa au huduma unazozitoa.

     Na blogu vile vile inakupa fursa ya kutangaza huduma na bidhaa zako kwao kwa njia isiyokera kwani ushakuwa mtu wao wa karibu mbele ya macho yao.

     Nimeelezea vizuri nukta hii katika video ifuatayo:

     Unaweza kumiliki blogu yako aidha kwa kulipia jina la domain yako (Domain Name ) yaani  www.jinalakampuni.com pamoja na kulipia eneo la kurusha tovuti hio (hosting).

     Kama hali ya kiuchumi sio mzuri, unaweza ukajisajili blogu ya bure kupitia huduma kama WordPress.com au Blogger.com. Ila tambua kuwa blogu hiyo haitokua chini miliki yako na muda wowote inaweza ikafungwa endapo utakiuka taratibu zao
    3. Jisajili Katika Mitandao Tofauti ya Kijamii, Sambaza Blogu Yako na Ushiriki Katika Mazungumzo na Wateja Wako / Wateja Wako Watarajiwa

     Social Media Ulimwengu Wa WhatsAppBaada ya kuwa na blogu, anzisha kurasa za biashara yako katika mtandao wa Facebook, Twitter, LinkedIn na kama upo Tanzania ingia Jamii Forums.

     Sambaza makala zako za blog yako kwenye mitandao hiyo kwa ajili ya kuanzisha mazungumzo na wateja wako watarajiwa na ujibu maswali watakayokuuliza.

     Huu hapa mfano:Kwa nini wafanyabiashara wa kiTanzania wanangaika kupata wateja kwenye mtandao.

     Na huu:
     Kosa Kubwa La Wafanyabiashara Wakitanzania

     Kama una kampuni yenye kutoa huduma kwa wateja wengi, kuanzisha mazungumzo ya huduma kwa wateja (customer care) yenye kusikiliza malalamiko ya wateja wako itasaidia sana kukuza brand na biashara yako kwa ujumla.

     Vodacom na Startimes wanafanya hivyo katika Jamii forums kama uonavyo hapo:Vodacom & Startimes Customer Support

     Au kama unataka kujenga ukaribu zaidi unaweza kuzungumza na wafuasi wako kupitia video kwenye Facebook wapate kukuliza maswali kuhusu vitu tofauti tofauti.

     Naona Vodacom wanafanya hivyo katika ukurasa wake wa Facebook kama uonavyo hapo:
     Vodacom-facebook

    4. Tengeneza Listi Ya Wateja Watarajiwa (Lead Generation):

     Blogu na mitandao ya kijamiiWataalamu wa masoko ya mtandao wana msemo unaosema:

     “The Money Is In The List”

     Yaani,

     “Pesa Zimo Kwenye Listi Ya Wateja Watarajiwa”

     Utafiti uliofanya na …… unaonyesha kuwa …….. ya watu watakaotembelea tovuti yako hawatorudi tena.

     Kama mfanyabiashara mwenye kujali maendeleo ya biashara yake, unatakuwa kuhakikisha watembeleaji wengi wa tovuti yako wanarudi tena na tena na tena kila unapochapisha makala mapya au unataka kutoa OFA mpya.

     Kufanya hivyo unatakiwa kupokea taarifa zao za mawasiliano yaani Jina na barua pepe.

     Ila tambua kuwa hakuna mtu atakayekupa taarifa zake za mawasiliano bure bure. Lazima uwaahidi kitu cha thamani ndipo watakubali.

     Kwa mfano sisi hapa kwenye tovuti yetu tunagawa kitabu cha “Masoko Facebook” BURE, kitabu ambacho kinawafundisha wateja wetu watarajiwa jinsi gani ya kupata wateja wengi kupitia mtandao wa Facebook kama unavyoona hapo chini.

     Masoko Facebook
     Na baada ya kuwa na taarifa zao (Jina na Barua pepe) tunakuwa na fursa ya kuwasiliana nao mara kwa mara kuwajuza kuhusu makala au OFA mpya.

     Kwa hivyo kama una tovuti yako na hukusanyi taarifa za wateja wako watarajiwa, mwambie mtaalamu wako wa kutengeneza tovuti (web designer) akufanyie hivyo sasa hivi.

     Au kama unataka ushauri zaidi kuhusu hili wasiliana nasi hapa.

    5. Tangaza makala zako kuwafikia Watu Wengi Zaidi:
     Kama una nia ya kuwasaidia watu wengi kufaidika na taaluma yako, basi unawajibika kwa namna moja au nyengine kusambaza ujumbe wako kwa watu wengi iwezakanavyo.Na kufanya hivyo inabidi utenge bajeti kwa ajili ya matangazo. Unaweza ukaanza kuweka matangazo kweny mtandao wa Facebook kwani gharama zake ni za chini na ni rahisi kuwafikia watu wengi hususan kama makala yako ni yenye kuvutia. Soma kitabu changu cha Masoko Facebook kujifunza zaidi.

     Pata Makala Yako Ya Masoko Facebook Bure
     Huu hapa ni mfano wa tangazo la makala yangu niloweka kwenye Facebook. Lilinigharimu $5 lakini limeonekana mbele ya macho ya watu 28, 489 na kati ya hao 995 wamesoma makala hiyo.Nimefafanua kiundani kwenye kitabu cha Masoko Facebook mbinu niliotumia kuweza kutumia gharama ndogo kwenye tangazo hilo.
     tangazo fb dola 5

Kwa hivyo ukifuata mbinu hizi nilizozieleza hapa (hata kama sio zote) kujenga biashara yako katika ulimwengu huu wa mitandao ya kijamii itakuwa ni jambo rahisi sana kwako.

Asante sana kwa muda wako. Natumai umejifunzi mawili matatu.

Nitafurahi sana ukifanya mambo yafuatayo:

 1. ‘Like’ makala hii kwa kubofya kitufe cha Facebook kilichoandikwa ‘Poa’.
 2. Niandikie ujumbe fupi ya kitu gani umejifunza kwenye makala hii na ungependa niongelee kitu gani kwenye makala zijazo.
 3. Na kama una swali lolote unataka kuniuliza, usisite kufanya hivyo.

Tuonana tena kwenye makala, video au ana kwa ana.

Peace!


Ujumbe Wa Facebook

Leave a Reply

Your email address will not be published.