Hivi hushangazwi kwanini kuna baadhi ya wafanyabiashara kila wanapotoa bidhaa au huduma kwenye soko wanakuwa wanauza kupindukia hali ya kuwa wewe unahangaika kama punda bila ya mafanikio yoyote?

Hivi ushawahi kujiuliza wafanyabiashara hawa wenye mafanikio wana siri gani?

Kama ushawahi lakini hukuwahi kupata jibu basi leo nataka nikupe siri ya wafanyabiashara hao.

Na siri yenyewe haihusiani na wao kufanya kazi kwa bidii wala kuwa na mtaji mkubwa.

Inatokana na sifa waliokuwa nayo ambayo wafanyabiashara wengi hawana.

Wafanyabiashara wanaohangaika ni watu ambao ni ‘instrinsic‘.

Yaani watu waliozungwa na dunia yao.

Zaidia ya 90% ya muda wao wanakuwa wanajifikiria wao na matatizo yao.

Wanawaza kuhusu familia zao, vipato vyao, bidhaa zao na jinsi ya kuziuza, ndoto zao n.k.

Kwa lugha nyengine tunaweza kusema wao ni ‘self-centred‘.

Ki ufupi dunia yote inamzunguka yeye.

Hakuna ubaya kuwa mtu wa dizaini hiyo ila ukiwa hivyo itakuwa viguma sana kupata mafanikio makubwa kwenye biashara yako.

Na siri ya wafanyabiashara wenye mafanikio makubwa ni kuwa wao ni ‘extrinsic‘.

Wanatumia 90% ya muda wao kufikiria matatizo ya wateja wao na jinsi ya kutatua matatizo hayo.

Na ndio maana unakuta wafanyabiashara kama Said Salim Bakhressa wanapotoa bidhaa katika soko linapokelewa vizuri na watu wengi wanaikubali.

Anaelewa matatizo ya wateja wake kiundani na anajua bidhaa au huduma gani itasaidia kutatua matatizo yao.

Wafanyabiashara wa namna hii huwa wanaamka kila siku na kujiuliza…

wateja wangu wana matatizo gani?

Nitengeneze bidhaa au huduma gani itakayotatatua matatizo yao?

Na sio…

nifanye nini nipate kuuza bidhaa yangu?

Kwani wafanyabiashara wenye mafanikio makubwa wanaangalia matatizo ya wateja wao kabla ya kutengeneza/kumiliki bidhaa.

Na ndio maana mhamasishaji maarufu, Tony Robbins anasema

“Do not fall in love with your products.
Fall in love with your customers”

Yaani,

“Usijenge mapenzi na bidhaa au huduma unazotoa.
Jenga mapenzi kwa wateja wako.”

Kwani mteja ndie mwenye kuendesha uchumi wa biashara yako.

Kwa hivyo ujumbe wango kwako ni nini?

Ujumbe wango kwako ni…

Punguza kuwaza matatizo yako.

Hakuna mtu atanunua bidhaa kutoka kwako kwa sababu mwanao anadaiwa ada ya shule.

Watanunua bidhaa / huduma kutoka kwako kwa sababu yatatatua matatizo waliyonao wao.

Elewa matatizo ya wateja wako na jifunze namna ya kutatua matatizo hayo.

Ongea na wateja wako.

Waulize…

Unasumbuliwa na kitu gani katika ……. (eneo la biashara yako)

Ukishapata jibu jiulize na wewe…

bidhaa au huduma gani naweza kuwauzia wateja wangu itakayoweza kutatua matatizo yao?

Ukishapata jibu, tafuta bidhaa au huduma yenye kutatua matatizo ya wateja wako.

Na ukifanikiwa kufanya hivyo, utakuwa umeingia katika kundi la 10% ya wafanyabiashara wenye mafanikio makubwa.

Na ukiendelea kutatua matatizo ya wateja wako kila siku, matunda ya kazi yako utayaona.

Na hilo ndio lengu kuu la biashara, ‘kutatua matatizo ya wateja wako.

Brian Tracy, Kocha wa wafanyabiashara na mhamasishaji maarufu ana msemo wake anaosema,

Making money is NOT the goal of your business. It is an outcome.

The goal of your business is solving problems.

Yaani…

Kutengeneza pesa sio lengo la biashara yako. Kutengeneza pesa na matokea ya lengo lako.

Lengo la biashara yako ni kutatua matatizo ya wateja wako.

Natumai umepata mawili matatu.

Kama una swali uliza kwa ku comment hapa chini.

Na kama utapenda kujifunza ‘Jinsi Ya Kutumia Mtandao Kunasa Wateja Kama Smaku’ BOFYA HAPA

Na nisaidie ku ‘share’ kwenye mtandao wa Facebook na WhatsApp kwa kwa kubofya kitufe husika hapo chini. ili na wao wafaidike.

Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako,

Dr. Said Said
CEO – Online Profits

NB: Kumbuka – Unastahili kuwa na mafanikio


Ujumbe Wa Facebook