Kama wewe ni mfanyakazi au mfanyabiashara na haijalishi unafanya biashara gani, aidha

unafanya Network Marketing, au Una duka lako unauza nguo au wewe ni Daktari au ni Mhandisi (Engineer),

au kazi yoyote  nyingine unayofanya basi nifuatilie kwa makini sana katika makala hii. Kwani ninaenda

kukuonyesha jambo muhimu sana kwako. Kabla sijakuambia jambo hilo angalia tatizo kubwa lililopo katika jamii.

Tatizo kubwa ninaloliona katika jamii ni kuwa watu wengi wanataka kujifunza mambo mengi

badala ya kujifunza mambo machache na kuzama ndani juu ya mambo hayo machache na huenda wewe

unayesoma makala hii ukawa mmojawapo.

Bruce Lee aliwahi kusema “Simwogopi mtu aliyejifunza mateke elfu kumi bali

namwogopa mtu  ambaye amejifunza teke moja mara elfu kumi”.  Kwa nini alisema hivyo?,

Sababu ni kwamba mtu aliyejifunza teke moja mara elfu kumi anakuwa amemaster kile kitu kuliko mtu yoyote.

Siku hizi tuna vyanzo vingi vya taarifa na maarifa, idadi kubwa ya watu wanasoma vitabu vingi

lakini wanachokijua katika wanayoyasoma ni maarifa machache tu ya juu juu na sio kwa undani.

Kama unataka kuzama ndani katika kile unachokisoma basi unatakiwa uchukue taarifa uliyoisoma,

uiweke katika utekelezaji na unaifanyia mazoezi, unaijaribu katika soko mpaka unakuwa

mtaalamu wa kile kitu, na hili ndilo jambo ambalo limekosekana kwa wafanyabiashara wengi.

Unaweza kukutana na mtu ambaye amesoma vitabu vya Success (Mafanikio) lakini anahangaika, kwa nini?,

Sababu ni kwamba anakusanya maarifa mengi badala ya kufocus taarifa chache ambazo atazifahamu kwa

undani na kuzifanyia kazi.

Mfano mzuri kuna kitabu kinaitwa Think and Grow Rich, Kitabu hiki kinasemekana ndio  kitabu

kilichozalisha matajiri wengi Duniani kuliko kitabu kingine chochote, kama umesoma hiki kitabu

na hakuna hatua uliyopiga katika maisha yako, na ukasoma kitabu kingine labda umesoma Rich

 Dad, Poor Dad na  haujapiga hatua katika maisha yako na ukasoma kitabu kingine labda How To

Win Friends and Influence People na bado haujapiga hatua yoyote katika maisha yako, hapo

unatakiwa upunguze kusoma vitabu na uchague kitabu kimoja na uchukue kile kitabu uhakikishe

unapiga hatua kupitia hicho kitabu na usonge mbele mpaka uone kitabu hiki kimeshanifikisha

mpaka hapa sasa nahitaji kitabu kingine.

Na njia nzuri ya kukusanya taarifa niliyojifunza ni kwamba ujue kwanza unataka nini, na una

malengo gani?  Na uamue unataka kumaster kitu gani, kwa mfano unataka kuwa mtaalamu katika

Facebook Marketing, Kwa hivyo jambo la kwanza ni kujiuliza kuna vitabu gani vinavyohusu

Facebook Marketing ninavyotakiwa kusoma na hutakiwi kusoma kitabu kingine chochote

isipokuwa kinachohusu Facebook Marketing, hapo ndio unazama katika Marketing. Swali la pili

ni nani anayefanya Facebook Marketing anifundishe au niweze kununua kozi yake, nani atakuwa

Mentor (Mshauri) atakayeniongoza katika masuala ya Facebook Marketing kwa hiyo hapo

unazama ndani zaidi katika topic moja. Ukishafikia hatua ambayo umeridhika katika Facebook

Marketing na unataka kwenda hatua nyingine basi tafuta taarifa ambayo itakupeleka katika hatua

nyingine. Tatizo ninaloliona kwa watu ni kusoma taarifa nyingi kwa wakati mmoja bila kuzifanyia

kazi. Unakuta mtu anasoma Facebook Marketing, muda huohuo anasoma Bitcoin, muda huohuo

anasoma Investing (Uwekezaji), anasoma Success, akili yake inamdanganya kuwa anafanya kitu

sahihi lakini si hivyo bali anajiumiza mwenyewe.

Najua wengi wanaweza wasipende kuambiwa ukweli huo lakini huo ndio uhalisia. Kwa hiyo

jambo la muhimu ni kuzama zaidi katika jambo moja badala ya kuhangaika na mengi.

Pia kama ungependa kutumia mtandao wa Facebook na Instagram kunasa wateja kama sumaku, basi tumeandaa kozi ya nzuri kwa ajili yako. Kuanza kusoma Kozi hiyo Bofya Hapa

 

 


Abdallah Hemedi
Abdallah Hemedi

Content Manager

Ujumbe Wa Facebook

Leave a Reply

Your email address will not be published.