Hatua 1: Jiandae Kupata Mafanikio
Ndani ya eneo hili tutazungumzia kiundani jinsi ya kujiandaa kisaikolojia kuweza kupata mafanikio. Bila ya kujenga nguvu ya nafsi, kupata mafanikio kwenye mtandao (au kitu chochote kile) itakuwa ngumu mno.
Utangulizi
Muda wa Video: 6:16
Ndani ya video hii utajifunza sifa 6 (kutokana na utafiti uliofanywa na Brendon Burchard) za muhimu kuzingatia kuweza kupata mafanikio.
Bonus na Mazoezi ya Kufanya
1: Nunua kitabu cha High Performance Habits Hapa au sikiliza masimulizi ya kitabu BURE hapa
2: Pima uwezo wako wa kupata mafanikio hapa >> High Performance Indicator
3: Share na sisi majibu ya zoezi lako kwenye group la whatsapp hapa.
Mambo 3 Muhimu ya Kufanya Kila Siku
Muda wa Video: 8:41
Ndani ya video hii utagundua mambo 3 muhimu ya kufanya kila siku yatakayokusababisha kupata mafanikio kwa urahisi na kwa haraka.
1: Tafuta Ubayana [Seek Clarity]
Muda wa Video: 24:14
Ndani ya video hii utajifunza jinsi ya kuwa na bayana kuhusu wewe na ndoto zako, njia za kufuata kufikia malengo yako, kipaji chako na hisia unazotaka kuwa nazo kabla ya kupata mafanikio.
2: Zalisha Nishati [Generate Energy]
Muda wa Video: 21:02
Ndani ya video hii utajifunza njia za kisaikolojia za kutumia kuhakikisha unapata nishati (energy) kabla ya kufanya jambo lolote.
3: Kuza Uhitajio Wako wa Kupata Mafanikio [Raise Necessity]
Muda wa Video: 29:41
Ndani ya video hii utajifunza jinsi ya kukuza uhitajio wako wa kupata mafanikio. Unaona kwanini unahitaja mafanikio sasa kuliko muda wowote
4: Ongeza Ufanisi wa Kazi Yako [Increase Productivity]
Muda wa Video: 18:48
Je utapenda kujifunza namna ya kufanya kazi ya wiki ndani ya siku 1 na kazi ya mwezi ndani ya wiki 1? Ndani ya video hii utajifunza njia za uhakika za kuongeza ufanisi wa kazi zako.
5: Boresha Uongozi Wako [Develop Influence]
Muda wa Video: 15:17
Ndani ya video hii utagundua umuhimu wa kuwa kiongozi na unatakiwa kufanya nini kuweza kuwaongoza watu (timu yako pamoja na wateja wako watarajiwa) kuweza kupata mafanikio makubwa.
6: Kuwa Shujaa [Demonstrate Courage]
Muda wa Video: 19:00
Ndani ya video hii utagundua kwanini kuwa shujaa kutakusaidia kupata mafanikio kwa kiasi kikubwa mno. Vile vile utajifunza unatakiwa kufanya nini ili kuwa mtu shujaa.