Hatua 2: Elewa Upo Katika Biashara Gani
Ni wafanyabiashara wachache wanaoelewa wapo katika biashara gani. Wengi wao wanafikiria biashara yao ndio bidhaa au huduma wanazotoa lakini ni huo ni mbali kabisa na ukweli. Kuelewa biashara yako ndio msingi wa kuona mafanikio.
1: Utangulizi
Muda wa Video: 4:13
Ndani ya video hii utaona muhtasari wa mambo utakayojifunza katika hatua hii ya 2 ya kufahamu biashara yako.
2: Fanya biashara inayokufaa wewe
Muda wa Video: 16: 56
Ndani ya video hii utagundua mambo 3 ya kuzingatia kuweza kujua biashara gani itakufaa wewe.
3: Je biashara yako italipa na itadumu?
Muda wa Video: 12: 59
Ndani ya video hii utagundua mambo 4 ya msingi ya kuzingatia kuweza kumiliki biashara yenye kulipa na kudumu.
4: Lengo la biashara yako
Muda wa Video: 7:25
Wajasiriamali wengi wanadhani kuwa lengo kuu la biashara ni kutengeneza pesa. Hii ipo mbali na ukweli. Ndani ya video hii utapata kuelewa lengo kuu la biashara yako ni nini na kwanini kutumiza lengo hili utawavutia wateja wengi mno.
5: Mteja Wako ni Nani [Customer Avatar]
Muda wa Video: 16:03
Ndani ya video hii utapata kufahamu jinsi ya kutengeneza sifa za mteja wako mtarajiwa (customer avatar).
6: Utafiti wa soko lako [Market Research]
Muda wa Video: 11:13
Ndani ya video hii utajifunza jinsi ya kufanya utafiti wa soko lako (market research) kabla kuingia na kutoa ofa katika soko lolote. Utajifunza wateja wako wako wapi na wanahitaji nini n.k.