Watu wengi ambao hawajazama ndani ya  biashara wana picha fulani ya kwamba biashara au ujasiriamali ni

sehemu bora ya wao kuwepo. Kwa wengine inaweza kuwa sehemu nzuri kuwepo lakini wengi wanahangaika

katika biashara mpaka wengine wanajikuta wanataka kuutoa uhai wao kabisa. Hilo linatokana na

stress/msongo wa mawazo unaotokana na biashara.

 

Jambo muhimu na la msingi unalotakiwa kufahamu ni kwamba kazi kubwa ya Mjasiriamali au

mfanyabiashara ni kutatua matatizo ya watu, na uwezo wako wa kutatua matatizo ndio utakaokuwezesha

kupata mafanikio, kila unavyotatua matatizo makubwa zaidi ndivyo unavyozidi kupata mafanikio makubwa.

Kwa hivyo mfanyabiashara akiamka jambo la kwanza analotakiwa kujiuliza ni kwamba “Leo nina matatizo

mangapi ya kuyatatua?”  Na sio rahisi kwani kila ukiwa na matatizo mengi ndio msongo wa mawazo unavyoongezeka.

 

Kwa mfano nimewahi kukutana na msongo wa mawazo baada ya tovuti za wateja wetu zaidi ya 10

zilipodukuliwa (hacked). Hii ilinipa wakati mgumu sana kwani sikuwahi kukutana na hili tatizo kabla na pili

nilikuwa sijui nichukue hatua gani kutatua tatizo hili kwa kuwa ni jambo ambalo sikuwahi kufanya, Kwa hivyo

nilipata msongo wa mawazo wa hali ya juu. Lakini niliitisha kikao na wafanyakazi wangu kwa ajili ya kutafuta

suluhisho. Lakini kabla ya kutafuta suluhisho ilinibidi kuwapigia simu wenye tovuti kuwajulisha kuwa tovuti

zao zimedukuliwa kabla ya wao kutupigia sisi. Na tulifanikiwa kulitatua tatizo hili ndani ya masaa 24.

 

Na kila siku unajikuta una tatizo la kulitatua, na muda mwingine wafanyakazi wanapata matatizo unatakiwa

kuwasaidia, muda mwingine serikali inadai kodi au mwenye ofisi anadai kodi, kwa hiyo kuna mambo mengi

yanayotokea ndani ya biashara yako ambayo yanaleta msongo wa mawazo. Hivyo unatakiwa ujue jinsi ya

kudhibiti stress ulizonazo, kwa sababu kama haujatengeneza fomula nzuri ya kudhibiti stress zako unaweza

ukajikuta kuwa upo katika kitu ambacho kinatakiwa kikupe furaha lakini kinakutesa.

 

Kuna wafanyabiashara wengi ambao biashara zao zinawaingizia pesa lakini stress wanazoendana nazo hadi

kuingiza pesa ni kubwa mno, Muda wote wapo kwenye simu wakigombana na watu, ni jambo ambalo linawaumiza watu wengi sana.

Na kama wewe upo katika biashara na upo katika hali hiyo na unashindwa kudhibiti hali hiyo basi biashara haikufai.

Kwa hiyo nifuatilie kwa makini sana kwani nataka nikupe hatua ambazo unaweza ukazifata ili kudhibit

msongo wa mawazo katika biashara.

Kabla sijakwambia hatua hizo, kwanza nataka ufahamu kwamba stress/msongo wa mawazo sio kitu kibaya,

bali ni ishara ya kutokea kwa jambo/kitu  ambayo kutokana na ishara hiyo unatakiwa kuchukua hatua ya

kukabiliana na hilo jambo au kukimbia. Kama utakabiliana nalo hapo stress itakuwa imekusukuma kuchukua

hatua na kama utaogopa kukabiliana nalo hapo stress itakuumiza na kusababisha matatizo zaidi.

 

 

Jinsi ya Kudhibiti Stress/ Msongo wa Mawazo

Hatua ya Kwanza

Ni kuielewa kuwa huo msongo wa mawazo unatokana na nini, Kwa hivyo chukua kalamu na karatasi

 

uandike, labda inatokana na kazi nyingi sana zimerundikana au kuna kazi ambayo ulitakiwa kuikamilisha

 

ndani ya muda fulani lakini muda unakaribia kufika na bado hujamaliza.

 

Ukishajua  stress yako inatokana na nini, na ushaandika. Kwa mfano stress yako inatokana na kuwa una kazi

nyingi na unatakiwa kuzikamilisha ndani ya muda husika. Unachotakiwa kufanya ni kuandika kila kazi/project

 

na mwisho wake (lini inahitajika). Kwa mfano Kazi ya kwanza inatakiwa baada ya siku 5, kazi ya pili inatakiwa baada ya wiki 1.

 

Hatua ya Pili

Fanya kitu kimoja kwanza mpaka umalize ndipo uende katika kazi nyingine. Kwa mfano katika kazi ulizonazo

kuna kazi unayotakiwa kuikamilisha  baada ya siku 5. Anza na hiyo kazi na usifanye kazi nyingine mpaka hiyo

ikamilike.

 

Hatua ya Tatu

Jiulize,  Nifanye nini ili niweze kumaliza hii kazi/project haraka na nani ninaweza nikamtafuta ili anisaidie

nifanye hii project haraka. Muda mwingine unahitaji mtu wa ziada wa kukusaidia kutatua tatizo lillilopo,

usibebe mzigo peke yako, unaweza hata kumchukua mtu kwa kumlipa. Kwa mfano sisi (Dr Said na Timu

Yangu) tulipopata tatizo la website za wateja wetu kudukuliwa tulilazimika hata kuwalipa watu nje ya nchi ili

waweze kutusaidia kutatua tatizo hili.

 

Kama umejikuta  kila mara unapata stress katika biashara yako basi wewe umekuwa unaendeshwa na watu.

Ili kuepuka hilo Tenga muda usiku au hata asubuhi mapema weka ratiba ya siku yako, kwamba leo  nitafanya

hiki na hiki na usiruhusu mtu kuharibu ratiba yako labda kuwe na dharura kubwa iliyojitokeza. Kwa kufanya

hivyo itakusaidia sana kuweza kudhibiti msongo wa mawazo na kuendesha biashara Yako Vizuri.

Pia kama ungependa kujifunza Jinsi ya Kutumia Mtandao wa Facebook na Instagrama kunasa Wateja, basi

tumekuandalia Video inayoelezea Jinsi ya Kutumia Mtandao wa Facebook na Instagram kunasa Wateja.

Kuangalia video hiyo Bonyeza hapa.


Abdallah Hemedi
Abdallah Hemedi

Content Manager

Ujumbe Wa Facebook

Leave a Reply

Your email address will not be published.